Makamu wa Rais awataka Watanzania kuomba toba kwa Mungu kwa matendo ya kikatili kwa watoto

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Philip Mpango ametoa wito kwa Watanzania kuomba toba kwa Mungu kwa matendo ya kikatili hususani kwa watoto na kuacha dhuluma dhidi yao, huku akiwasihi kutimiza mahitaji ya watoto katika kuwatunza ikiwemo kuhakikisha wanapata elimu.
Makamu wa Rais, Dkt.Philip Mpango akizungumza leo baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Sikukuu ya Krismasi katika Parokia ya Kristo Mfalme, Veyula mkoani Dodoma. Kushoto kwake ni Mama Mbonimpaye Mpango. (Picha na OMR).

Akizungumza leo Desemba 25, 2025 baada ya kushiriki Ibada ya Misa Takatifu ya Sikukuu ya Krismasi katika Parokia ya Kristo Mfalme, Veyula mkoani Dodoma, Makamu wa Rais pia ametoa wito kwa Watanzania kuongeza jitihada katika kuimarisha ulinzi wa watoto ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili vinavyowakumba.

Kuhusu mvua zilizoanza kunyesha hapa nchini, Makamu wa Rais pia ametoa wito kwa watanzania kutumia fursa ya uwepo wa mvua hizo katika kuzalisha mazao na kupanda miti ili kuhifadhi mazingira.
Waumini wakiwa kwenye Ibada hiyo. (Picha OMR).

Amesema, ni muhimu suala la upandaji miti kuanza katika ngazi ya familia kwa kupanda miti mitatu kila familia na hivyo kupendezesha nchi na kulinda mazingira.

Katika ibada hiyo, Makamu wa Rais ameambatana na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango na ibada imeongozwa na Paroko wa Parokia ya Kristo Mfalme iliyopo Veyula Dodoma Padre Saimon Katembo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news