PASIPO MUNGU MWANADAMU HAWEZI KITU-PADRI MAPALALA

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wameambiwa kuwa wanaposherehekea Sikukuu ya Krismasi wafahamu kuwa pasipo Mungu mwanadamu hawezi kitu chochote katika huu ulimwengu.

Hayo yamesemwa Disemba 24, 2022 na Padri Paul Mapalala katika mahubiri ya misa ya mkesha wa sikukuu hii katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata Parokia ya Chamwino Ikulu, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
“Wengine wanasherehekea sikukuu ya kuzaliwa mwokozi Yesu Kristo mara yao ya kwanza na wengine ni mara nyingi sana, hapo Mungu sote anatupa angalizo kuwa sisi binadamu maisha yetu siyo yetu bali ni yake mwenyewe kwa mapenzi yake.

"Kila mwanadamu ameumbwa kwa taswira ya Mungu kusudio ni kumuenzi Bwana wetu Yesu Kristo na kubwa ni kuendeleza utukufu wa Mungu katika maisha haya.”

Aliongeza kuwa, mwanadamu anapita katika majira mbalimbali na nyakati mbalimbali, lakini sote tutambue kuwa chanzo chetu ni Mungu mwenyewe.

Misa hiyo iliambatana na maombi kadhaa na mojawapo ni hili,
“Uliunganisha mbingu na Dunia, utuguse tutamani mambo ya mbinguni zaidi ya yale ya duniani.”

Mpaka Misa hii ya mkesha wa Krismasi inamaliza saa 5.00 ya usiku wa Disemba 24, 2022 mvua katika eneo la Chamwino Ikulu imenyesha kwa mfululizo kwa siku mbili yaani Disemba 23 na Disemba 24 huku wakazi wa eneo hili wameonekana wakipiga mashimo na kupanda mbegu za mazao mbalimbali ikiwemo mahindi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news