Makamu wa Rais:Viongozi wa namna hii hawatufai

NA MWANDISHI WETU

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango amesema, kuna baadhi ya viongozi kwa maslahi yao binafsi wanachangia katika uharibifu wa mazingira.
Dkt.Mpango ametoa kauli hiyo leo Desemba 19, 2022 mkoani Iringa katika Kongamano la Wahariri na Wadau wa Uhifadhi, Mazingira na Utunzaji wa Vyanzo vya Maji.

"Wapo baadhi ya viongozi kwa maslahi binafsi, wanachangia sana kwenye uharibifu wa mazingira.
"Siamini wakulima wetu masikini, wafugaji kwamba ndio wanaoharibu mazingira. Lazima tunusuru mito yetu yote hasa mito ya kimkakati kama Ruaha, viongozi wa namna hii hawatufai," amesema Dkt. Mpango.

Katika kongamano hilo amesema, mwaka 1980 uharibifu wa mazingira ulifanywa kwa asilimia 42; mwaka 1980 asilimia 50 na mwaka 2012 uharibifu ulikuwa kwa asilimia 68.
Kwenye kongamano hilo,Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), ameishauri serikali kuchukua hatua ya kuiondoa Ranchi ya Usangu ambayo ipo ndani ya bonde oevu linalolisha maji Mto Ruaha Mkuu sambamba na kujenga tuta eneo la Ngiliamu ili kuunusuru mto na ukame.

"Sisi tunafanya habari za uchunguzi na tumebaini Ranchi ya Usangu inamilikiwa na familia 12, wamo majaji, wamo wabunge, wamo mawaziri na leo nitakukabidhi majina.

"Ranchi hii ilifutwa na GN No. 28 lakini kamati ya mawaziri wanane iliamua kuiacha," amesema Balile.
Habibu Mchange ambaye ni Mwenyekiti wa MECIRA amesema, leo ni siku ya 130 Mto Ruaha hautiririshi maji.

"Leo Mto Ruaha Mkuu umefikisha siku 130 bila kutiririsha maji, na ukienda hifadhini utasikitika kuona viboko wanagombania mchanga na si maji kutokana na uharibifu wa mazingira,"amesema Mchange.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news