Meli ya Le Bougainville yatia nanga Doha, yaashiria kuanza kwa safari za meli za kitalii

DOHA-Mamlaka ya Bandari nchini Qatar (Mwani Qatar) imetangaza kuanza kwa msimu wa safari mwaka 2022-23 huku meli ya Ufaransa ya kitalii ya Le Bougainville ikitia nanga katika Bandari ya Doha leo.
Meli ya Le Bougainville ikitia nanga katika Bandari ya Doha nchini Qatar leo Desemba 25, 2022. (Picha na Mwani Qatar).

Pamoja na picha za meli ya kitalii na watalii wanaowasili Qatar, Mwani imefafanua kuwa, "Meli ya kitalii Le Bougainville ilitia nanga katika Bandari ya Doha leo kuashiria kuanza kwa msimu wa 2022/23."

Meli hiyo inasimamiwa na kampuni ya Ufaransa ya Ponant Cruises, ikiwa ni meli ya kwanza ya msimu huu ambayo ina urefu wa mita 131 na upana wa mita 18, inaweza kubeba watu 294, pamoja na wafanyakazi.
Katika msimu wa safari za meli, ambao huanza Novemba hadi Aprili kila mwaka, Bandari ya Doha huwa inapokea meli nyingi zikiwa zimejaa watalii kutoka pande mbalimbali za Dunia. 

Aidha, kuwasili kwa Le Bougainville inatajwa kuwa ni mwanzo wa kupokea meli nyingi zaidi za kitalii kuanzia sasa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news