Mfalme Al-Sultan atua Qatar kushuhudia Kombe la Dunia

NA DIRAMAKINI

MFALME wa Malaysia, Al-Sultan Abdullah Ri'ayatuddin Al-Mustafa Billh Shah amewasili Desemba 13, 2022 jijini Doha, Qatar kuhudhuria sehemu ya mechi za Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) 2022 Qatar.

Mtukufu Mfalme pamoja na ujumbe aliofuatana nao walipokelewa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad na Mheshimiwa Waziri wa Michezo na Vijana, Salah bin Ghanem Al Ali na Mheshimiwa Balozi wa Malaysia nchini Qatar, Zamshari Shaharan.

Kiongozi huyo na viongozi wengine kadhaa kutoka pande mbalimbali za Dunia huenda anatarajia kushiriki katika fainali za Kombe la Dunia siku ya Jumapili katika dimba la Lusail lililopo Doha nchini Qatar.

Argentina inatarajiwa kumenyana na mshindi wa mechi ya Ufaransa na Morocco ambao wanaumana leo Desemba 14, 2022 katika Dimba la Al-Bayt huko Al Khor, Qatar. (thepeninsula)

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news