Spika wa Baraza la Wawakilishi Misri atua Qatar kushuhudia Kombe la Dunia

NA DIRAMAKINI

SPIKA wa Baraza la Wawakilishi la Jamhuri ya Misri, Mheshimiwa Kansela Dkt. Hanafy El-Gebaly amewasili Doha Jumanne jioni kuhudhuria sehemu ya mechi za Kombe la Dunia la FIFA nchini Qatar 2022.

Mheshimiwa Spika, pamoja na ujumbe aliofuatana nao, walikaribishwa mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hamad na Spika wa Baraza la Shura, Mheshimiwa Hassan bin Abdullah Al-Ghanim, na Balozi wa Jamhuri ya Misri katika nchi ya Qatar, Mheshimiwa Amr El-Sherbini.

Spika huyo na viongozi wengine kadhaa kutoka pande mbalimbali za Dunia huenda anatarajia kushiriki katika fainali za Kombe la Dunia siku ya Jumapili katika dimba la Lusail lililopo Doha nchini Qatar.

Argentina inatarajiwa kumenyana na mshindi wa mechi ya Ufaransa na Morocco ambao wanaumana leo Desemba 14, 2022 katika Dimba la Al-Bayt huko Al Khor, Qatar.

Post a Comment

0 Comments