Mhandisi Zena asaini kitabu cha maombolezo Ubalozi Mdogo wa China Zanzibar

Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said akisaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa China, Jiang Zemin alipofia katika Ofisi ya Ubalozi wa Mdogo wa China uliopo Mazizini jijini Zanzibar leo Desemba 5, 2022.Kushoto ni Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China aliyepo Zanzibar, Mhe.Zhang Zhisheng.Rais wa zamani wa Jamhuri ya Watu wa China, Jiang Zemin, ambaye aliongoza nchi kupitia mabadiliko kisiasa mwishoni mwa mwaka 1980 alifariki dunia Novemba 30, 2022 akiwa na umri wa miaka 96.
Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said akisaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa China, Jiang Zemin, alipofika katika Ofisi ya Ubalozi Mdogo wa China uliopo Mazizini jijini Zanzibar leo.
Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said akizungumza na Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyia kazi zake Zanzibar, Mhe. Zhang Zhisheng baada ya kutia saini kitabu cha maombelezo kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa China, Jiang Zemin leo katika Ubalozi Mdogo wa China Mazizini Zanzibar.
Katibu Mkuu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Ahmed Said (katikati) akiagana na Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China anayefanyia kazi zake Zanzibar, Mhe.Zhang Zhisheng baada ya kutia saini kitabu cha maombelezo kufuatilia kifo cha Rais mstaafu wa Jamhuri ya Watu wa China, Jiang Zemin, leo katika Ofisi ya Ubalozi Mdogo wa China Mazizini Zanzibar, kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje, Ofisi ya Zanzibar, Bi.Mariam Haji Mrisho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news