Mheshimiwa Sagini ampa kongole Rais Dkt.Samia kwa kuweka mazingira mazuri ya wahamiaji nchini

NA DIRAMAKINI

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Jumanne Sagini ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya wahamiaji hapa nchini.
Amesema kuwa, hatua ya Rais Dkt.Samia kuweka mazingira mazuri ina faida kubwa kwa nchi, hivyo hatua hiyo amesema inapaswa kupongezwa kwani inachochea maendeleo na shughuli za uwekezaji.

Mheshimiwa Naibu Waziri Sagini ameyasema hayo Desemba 18, 2022 wakati wa kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wahamiaji Duniani ambapo kitaifa imeadhimishwa Kurasini jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Sagini pia amesema kwamba, Serikali itaendelea kuhakikisha usalama kwa wahamiaji waliopo nchini kwa taratibu za kisheria. Huku pia akizitaka taasisi zinazoshughulikia wahamiaji kuzitumia vyema fursa za uhamiaji wa binadamu kama chachu ya maendeleo.
Pia Mheshimiwa Sagini ameishukuru serikali kwa kufanya marekebisho ya kanuni ya Sheria ya Uhamiaji sura ya 54 rejeo la mwaka 2016.

Sambamba na Serikali kufanya mabadiliko ya Sheria ya Uhamiaji sura ya 54 kwa kupunguza ada ya kibali cha ukaazi wa wawekezaji wa nje wenye asili ya Tanzania (Diaspora) kutoka dola za kimarekani 3,050 hadi dola za Kimarekani 1,050 ili kuwahamasisha raia hao kuwekeza katika nchi yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news