Mna mchango mkubwa kuelimisha jamii masuala yahusuyo afya-Wizara ya Afya

NA DIRAMAKINI

WIZARA ya Afya imesema kuwa,inathamini kwa upekee mchango wa vyombo vya habari nchini kwani vimekuwa mstari wa mbele kuhakikisha vinasaidia kueneza taarifa chanya zinazohusiana na masuala ya afya ikiwemo namna ya kukabiliana na magonjwa mbalimbali kwa jamii.
"Vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kufikisha taarifa, na pia vyombo vya habari hutumia muda mfupi kuwafikia watu wengi zaidi katika jamii.

"Lakini wananchi wana imani na vyombo vya habari, na vyombo vya habari pia huwezesha watu kubadili tabia na kufanya maamuzi sahihi juu ya afya zao. Kwa hiyo, ninyi ni wadau muhimu sana kwetu;
Hayo yamebainishwa Desemba 10, 2022 jijini Dar es Salaam na Afisa Habari Mwandamizi wa Wizara ya Afya, Bi.Catherine Sungura katika mafunzo ya kuwajengea waandishi wa habari uelewa kuhusu namna bora ya kutoa elimu ya kukabiliana na ugonjwa wa Ebola iwapo utaingia hapa nchini.

"Ni muhimu kuimarisha mahusiano kati ya jamii na wataalam wa hospitali kwa sababu inapotokea mlipuko na dharura yoyote source of information (chanzo cha taarifa) ni Serikali, ninyi huwa mnakuja kwetu na mnapata taarifa sahihi.

Wajibu wao

"Nini wajibu wa vyombo vya habari wakati wa kukabiliana na ebola? Wajibu wa vyombo vya habari ni kuelimisha jamii kuhusu dalili za ugonjwa na jinsi ya kutoa taarifa, kukemea upotoshwaji na kutoa elimu ya habari sahihi kuhusu ebola.

"Hiki kipengele ni muhimu sana unapoandika taarifa sahihi, wewe unakuwa unakemea hivyo ni wajibu wa vyombo vya habari kuhimiza jamii kuzingatia njia za kujikinga na kuzuia maambukizi ya ebola, ninyi mlisaidia katika suala la UVIKO-19 na tukawa tunazingatia usafi binafsi na usafi wa mazingira kwa hiyo hiyo ni moja ya wajibu wenu.

"Pia, kusambaza habari zenye ujumbe wa kweli kuepusha upotoshaji. Kama nyie mtalega mkasambaza ujumbe usio mzuri mtakuwa mmepotosha jamii kwa sababu jamii inawaamini sana."

Wizara

"Sisi kama Wizara ya Afya tunatoa ujumbe mahususi kwamba ni muhimu kutoa taarifa sahihi na kuepusha upotoshaji, kuepuka kutoa tafsiri isiyo sahihi na kusababisha taharuki. Kwa sababu kama unaaminiwa ukatoa taarifa ya upotoshaji jamii yote itaogopa.
"Lazima kujifunza mambo mapya kuhusu ugonjwa wa ebola, tusisubiri tu kwamba tutapewa taarifa au kuingia kwenye website ya wizara, lakini kumbe tunapaswa kusoma, elimu haina mwisho WHO (Shirika la Afya Duniani) unaweza kuingia kwenye website yao kila mara wana updates (wanahuisha) vitu kwa hiyo ukiangalia kule ukajifuza kupita kalamu yako unatoa habari sahihi.

"Kujifunza jitihada za kutoa habari mapema kwa jamii, sio unatoa habari mapema ambayo sio sahihi ni bora ukatoa habari mapema kwa jamii iliyo sahihi na kuzingatia maelekezo ambayo mmepewa, tuibue mijadala yenye tija na kuleta suluhisho katika kukabiliana na Ebola iwapo itaingia nchini. Sisi Tanzania tunamshukuru Mungu hatujapata mgonjwa yeyote,"amesema Bi.Sungura.

Dkt.Hokororo

Naye Mratibu wa Kinga na Udhibiti Magonjwa ya Mlipuko kutoka Wizara ya Afya, Dkt.Joseph Hokororo amesema, lengo la kuwajengea uwezo wanahabari hao ni ili waweze kutumia kalamu zao vizuri kuelimisha jamii juu ya namna ya kukabiliana na magonjwa ya milipuko ikiwemo Ebola ambao haujaingia nchini.

"Sisi kama nchi tuweze kujipanga vizuri ugonjwa huu usienee iwapo utaripotiwa. Na ugonjwa huu upo tayari nchi jirani ya Uganda na mwingiliano kati ya Uganda na Tanzania ni kubwa kwa shughuli za kijamii na kiuchumi.

Habari njema

"Tunashukuru Mungu toka tarehe 27, mwezi uliopita hatujata taarifa za kesi mpya huko Uganda, kwa taarifa tulizonazo mpaka saas hivi, jumla ya kesi zote zilizokuwepo Uganda ni kesi 142 na kati ya hao 55 walifariki na kupelekea kuwa asilimia 38.7, lakini tukumbuke kulikuwa na kesi 22 hazikuwekwa kwenye hizi asilimia,ingekuwa zaidi ya asilimia 50.

"Huu ugonjwa kwa mujibu wa stadi mbalimbali na Shirika la Afya Duniani (WHO) ikitokea kati ya watu 100 maana yake watu 40-90 wanaweza kupoteza maisha.

"Sasa hivi tuna karibu siku 12 na ugonjwa huu unatangazwa rasmi haupo kwenye nchi mpaka zipite siku 21, kwa hiyo kama nchi (Uganda) wao wanaendelea kujipanga na kufuatilia mpaka siku 21 zifike zikishafika sasa wanaweza kutangaza ugonjwa huu umeisha.

Ufuatiliaji zaidi

"Kwa hiyo hata sisi vile vile tunaendelea kufuatilia kwa sababu bado kuna mwingiliano wanaokuja na kutoka ufuatiliaji wa kwenye mipaka bado unaendelea...na sisi kutokana na mwingiliano lazima tuwe makini kuhakikisha tunakabili ugonjwa huu usiweze kuingia nchini.

"Lakini ukiingia lazima tujipange, tumeshaandaa wataalam wetu, tumeandaa sehemu za kuweka wagonjwa na makundi mbalimbali tunaendelea kuyajengea uwezo, kuwaelimisha lakini pia kundi la wanahabari ni muhimu zaidi litatusaidia kufikisha jumbe mbalimbali kwa wananchi namna gani nzuri ya kujikinga na namna gani tunapeleka ujumbe mzuri ili tusipeleke taharuki kwa wananchi.

Umetoka wapi

"Ugonjwa huu umetokea nchi mbalimbali za Afrika hasa zenye misitu mikubwa, Kongo, Uganda, Sudan na kadhalika. Kama mlivyoona, yule mzee alianza kwenda kununua nyama za wanyama wa mwituni. Lakini mwanzo kabisa maambukizi yalianza kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu baada ya hapo sisi binadamu tukaanza kuambukizana.

"Hawa virusi wamegawanywa aina sita, familia sita za Ebola na majina haya wamepewa kutokana na unapotokea...kwa sasa hivi tuliyonayo ni ile ya Sudan, uzuri wa hii ni kwamba uambukizaji wake si wa kiasi kikubwa na hata usababishaji wa vifo sio mkubwa kama hizo aina zingine.

"Namna ambavyo huenezwa kwa kiasi kikubwa ni kutoka kwa wanyama aina popo, na jamii ya nyani,sokwe na lazima ugusane na vijidudu au products zake kama nyama, maji maji na baada ya hapo sasa ikishakuja kwa binadamu tunaanza kuambukizana sisi kwa sisi kwa kugusa, sana sana maji maji yakiwemo mkojo, kamasi.
"Lakini pia sisi binadamu wale wanaobahatika kupona wenyewe wanaweza kuwa wameshapona kinga ya mwili, hawawezi tena kuambukizwa, lakini bado wanaweza kuambukiza na kwa wanaume wataendelea kuambukiza zaidi ya miezi sita mpaka mwaka kwa kutumia njia ya kujamiana, kwa hiyo vijidudu vitaendelea kuishi kwenye shahawa kwa hiyo kipindi hicho mtu atatakiwa afanye safe sex kwa sababu bado kwenye shahawa kuna vijidudu.

"Lakini pia kina mama wanaonyonyesha wataendelea kuambukiza kupitia maziwa, kwa hiyo watoto wadogo nao wanaweza kuambukizwa kutoka kwa huyo mama aliyepata huo ugonjwa na akapona.

"Kama nilivyosema ni direct contact, lazima ugusane na mgonjwa kama mgonjwa aliacha maji maji yake kwenye siti, kiti, simu mike, ukigusa yale maji unapata ugonjwa huo. Sio tu lazima kugusana, lakini pia kugusa surface yoyote ile ambayo mgonjwa amegusa.

"Mimi ninaweza nikaambukizwa, lakini kama sina dalili siwezi kuambukiza kwa hiyo kuanzia pale ninapopata dalili ninaanza kuambukiza ugonjwa wa ebola katika zile siku 21. Kama nikianza kupata dalili siku ya pili, ya tatu au ya nne kuanzia hapo lazima nianze kuambukiza sio kama UVIKO-19, UVIKO-19 unaweza kuwa huna dalili, lakini ukaambukiza, lakini transmission nyingine ni ndio hiyo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na kimsingi yule anayenyonya.

"Kama nilivyosema mwanzo mliona ugonjwa ulivyoenea kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu baadaye tukaanza kuambukizana binadamu kwa binadamu.

"Kwa sisi ambao kazi zetu tunachangamana na watu mbalimbali kama wanahanari ambavyo mnakuwa kwenye harakati kwa watu mbalimbali kwa ajili ya habari na sisi ambao tunatoa huduma za afya mahospitalini, kwa hiyo tunakuwa kwenye risk (hatari) ya kupata maambukizi na mtu yeyote ambaye anafanya kazi katika mchangamano wa watu mbalimbali..

"Ugonjwa huu ulianza mwaka 1976 baada ya hapo nchi mbalimbali zikaanza kupata huu ugonjwa na ukishapata huu ugonjwa dalili ni kama vile ilivyo dalili za malaria yaani homa, uchovu, unakosa hamu ya kula misuli inauma, kichwa kinauma unajisikia kichefu chefu unaweza kuharisha hizo ni dalili za kwanza.

Fahamu

"Na kipindi hiki ni hatari zaidi watu wanaweza kufikiria ni malaria, typhoid, kwa hiyo chances za wewe kuchangamana na wengine, lakini pia utaenda hospitali, wauguzi nao wanaweza kupata maambukizi wanaweza kudhani kwamba ni ugonjwa mwingine na sio ebola na ndio changamoto ya ugonjwa huu mpaka inapofikia na mpaka inafikia stage ya pili ambapo complication zimeanza maini, figo zinaanza kushindwa kufanya kazi.

"Kwa sababu tunajua maini yanazalisha zile chembe ambazo zinasaidia ugandishaji wa damu, kwa hiyo yanaposhindwa kufanya kazi na system nzima ya mwili ya namna ya kugandisha damu inashindwa ndio sasa damu sehemu yoyote yenye upenyo.

"Ni jukumu muhimu kuhakikisha mgonjwa wa Ebola anatengwa na si kwamba tunamnyanyapaa, lakini ni namna nzuri ya kuhakikisha hasababishi maambuzi.

"Na ndio maana sasa hivi tumetoa maelekezo kila halmashauri iwe na sehemu ya kutoa huduma wakipata tu mgonjwa wanapeleka kwenye kituo. Kwa Dar es Salaam tumependekeza Temeke na Kipawa hizo ndizo sehemu zitakuwa zinatoa huduma kwa (ebola cases), kwa hiyo lazima tuhakikishe tunawatenga sehemu wasiweze kuambukiza wengine.

"Lakini kwa kadri ya maelekezo ya Shirika la Afya Duniani ili kuonesha kwamba wagonjwa wetu hawawi na stress unajua wakati mwingine ukipata msongo wa mawazo unaweza kufanya ugonjwa ukawa mkubwa zaidi na ukapoteza maisha ili kuondoa msongo wa mawazo wenzetu wa Shirika la Afya wanapendekeza kwamba watu waweze kuwaona hao wagonjwa, lakini katika mazingira ambayo hayataleta maambukizi...

"Kwa hiyo unaweza kuongea na wagonjwa watu wakawaona. Lakini mgonjwa wa Ebola anapata dalili kama malaria, Typhoid, UTI...kitu kikubwa ambacho tunakifuatikia ni kama mtu huyo ana dalili hizo na anatokea kule ambako ugonjwa upo Uganda, kwa hiyo sio kila mtu anayetoka damu ana ebola hapana, kwa hiyo lazima pawepo na uhusiano vinginevyo mpaka tukiwa na mgonjwa nchini.

"Suala la dawa,kuna dawa ambazo zinaendelea kufanyiwa majaribio, tunasema kuna dawa za ina mbili, lakini bado hazijatangazwa rasmi...lakini kuna dawa ambazo zinaendelea kufanyiwa kazi na zimesaidia hasa kupunguza vifo vya wagonjwa.

Maabara

"Kwa sasa hivi maabara yetu ya taifa inaweza kufanya moja ya vipimo na pia maabara zinazotembea Kagera kwa sababu kama mnavyojua unaweza ukahisiwa na kama ukihisiwa hutatakiwa tena kuchangamana na wengine, lazima ufanyiwe vipimo na upate majibu mapema ukichelewa kupata majibu unaweza ukawekwa sehemu ambayo umetengwa muda mrefu,jambo ambalo si jema.
"Kuna mambo ya mahusiano, magari ya kusafirisha wagonjwa au maiti, lakini vifaa vya kufanyia usafi, vifaa vya kujikinga kutoa taarifa kwa jamii chanjo kati ya zile familia sita tulizoziona za ebola. Kuna zingine zina chanjo ila Shirika la Afya Duniani wanajaribu kupambana kuona kama kuna uwezekano wa kuja na tiba.

"Binadamu anaambukiza ugonjwa huu pale ambapo anapokuwa na dalili mtu akizidiwa mapema chance ya kupona ni kubwa kuliko kuchelewa kwa sababu ukichelewa itapelekea maini, figo visifanye kazi. Vijidudu hivi stadi zinaonesha kwamba haviwezi kuishi nje ya majimaji,"amefafanua kwa kina Mratibu wa Kinga na Udhibiti Magonjwa ya Mlipuko kutoka Wizara ya Afya, Dkt.Joseph Hokororo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news