Morocco yawang'oa Uhispania kwa mikwaju ya penalti baada ya 'utasa'

NA DIRAMAKINI

ACHRAF Hakimi ambaye ni mchezaji aliyezaliwa jijini Madrid nchini Uhispania ameiondoa Uhispania kwenye Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) 2022 nchini Qatar kwa kuipa ushindi wa kihistoria Morocco.

Achraf Hakimi akiweka kombora nyavuni kupitia penalti ya ushindi kwa Morocco.(Picha na Karim Jaafar/AFP).

Hakimi alifunga mkwaju wa penalti na kupelekea Uhispania kujikuta wakisalimu amri kwa Morocco, hivyo Morocco kutinga robo fainali ya kombe hilo kwa mara ya kwanza.

Ni kupitia mtanage ambao umepigwa Desemba 6, 2022 katika Dimba la Education City lililopo Doha nchini Qatar ambapo timu hizo zilicheza soka la aina yake.

Morocco na Uhispania zilipiga dakika 90 ambazo zilitamatika pande zote ubao ukisoma sufuri, huku dakika za nyongeza 30 zikipigwa ubao ukaendelea kusoma sufuri. Baada ya wawili hao kutoshana nguvu, iliamuliwa ipigwe mikwaju ya penalti ambapo Wamorocco walishinda 3-0.

Kocha wa Uhispania Luis Enrique alikuwa amedai kuwa, wachezaji wake walijiandaa kwa kupiga penalti 1,000 kama fundisho, lakini Pablo Sarabia, Carlos Soler na Sergio Busquets wote walikosa nafasi hiyo na Hakimi mzaliwa wa Madrid aliwafanyia ukatili.

Kikosi cha Walid Regragui ambacho kilifuzu 16 bora mwaka 1986 huko Mexico kwa kupata ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Canada kitamenyana na Ureno siku ya Jumamosi katika dimba la Al Thumama baada ya kuitafuna Uswisi kwa mabao 6-1.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news