Ureno yatinga Robo Fainali Kombe la Dunia 2022 kibabe, yawalaza Uswisi 6-1

NA DIRAMAKINI

GONCALO Ramos amepiga 'hattrick' ya kuvutia katika michuano ya Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) 2022 huku Ureno ikiwalaza Uswisi kwa mabao 6-1.
Ni kupitia mtanage wa nguvu ambao umepigwa Desemba 6, 2022 katika Uwanja wa Lusail uliopo Doha nchini Qatar na kutinga hatua ya robo fainali dhidi ya Morocco.

Kocha wa Ureno, Fernando Santos alikuwa amemuweka Cristiano Ronaldo benchi, huku Ramos akianza nafasi yake.

Mchezaji huyo wa Porto hakufanya makosa kufunga bao la kwanza dakika 17 tu kabla ya mabao mengine mawili kwa maana ya dakika ya 51 na 67 ya kipindi cha pili kuhalalisha uamuzi wa Santos ulikuwa sahihi.
Pepe alikuwa ndiye nahodha wa Ureno katika mtanange huu. (Picha na Sorin Furcoi/Al Jazeera).

Mkongwe Pepe dakika ya 33 alitupia kitu nyavuni, Raphael Guerreiro dakika ya 55 naye alichana nyavu, na mchezaji wa akiba Rafael Leao dakika ya 92 ya mchezo huo akivuruga mipango ya Uswisi kwa kupachika bao la sita.

Hadi mtanange unafikia tamati, A Selecao walikuwa na ushindi mnono. Aidha, Manuel Akanji alipata bao la kuwafariji Uswisi dakika ya 58, ambao walishindwa kufuzu kwa robo fainali ya mchuano mkubwa kwa mara nyingine tena.

Kwa matokeo hayo, Ureno sasa itamenyana na timu iliyosalia ya Afrika kwa manaa ya Morocco, Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Al Thumama uliopo Doha nchini Qatar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news