Pele aishukuru Qatar, wafuasi wake kwa heshima

NA DIRAMAKINI

GWIJI wa soka wa Brazil,Edson Arantes do Nascimento (Pele) ameishukuru Serikali ya Qatar na wafuasi wake kwa jumbe alizopokea wakati wa ziara yake katika hospitali moja nchini Brazil kwa uchunguzi wa kila mwezi.
Katika Instagram yake,gwiji huyo mwenye umri wa miaka 82 alichapisha picha ya Mnara wa Lusail uliopambwa kwa picha yake na maandishi ya 'Get Well Soon' kwa upande mwingine.

Pele, mchezaji pekee katika historia kushinda Kombe la Dunia mara tatu amekuwa akikumbana na matatizo ya kiafya katika miaka ya hivi karibuni, lakini mara nyingi huwa anawasiliana na wafuasi wake kupitia mitandao ya kijamii.

Pele, alicheza kama mshambuliaji wa kati na aliisaidia Brazil kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1958, 1962 na baadaye tena mwaka 1970.

Pia aliweka rekodi mwaka 1958 ya kuwa mchezaji mdogo kuliko wote duniani kucheza katika fainali ya Kombe la Dunia alipocheza akiwa na umri wa miaka 17 na alivuma sana katika miaka ya 1970 duniani kote.

Pele aliandika kwenye Instagram: "Marafiki, niko hospitalini nafanya ziara yangu ya kila mwezi. Daima ni vizuri kupokea jumbe chanya kama hizi. Asante kwa Qatar kwa heshima hii, na kwa kila mtu anayenitumia jumbe nzuri!"

Kipimo cha Pele cha Instagram pia kinamuelezea kama, Mfungaji Bora wa Muda wote (1,283), Mchezaji wa FIFA wa Kandanda wa Karne, na Balozi wa Kimataifa na Mfadhili wa Mahitaji ya Kibinadamu.

Sanamu kubwa ya Pele inaoneshwa kwa sasa katika Onesho la Shirikisho la Soka la Amerika Kusini (CONMEBOL) huko Msheireb jijini Doha kama sehemu ya sherehe za Kombe la Dunia la FIFA la Qatar 2022 ikiangazia historia ya maisha yake.

Mchango wake na kumbukumbu zingine za kandanda zinaoneshwa kwa mashabiki kuona na kupiga picha kuanzia asubuhi hadi usiku.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news