Rais Dkt.Mwinyi azindua Studio za Wasafi FM jijini Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi Media,Abdul Nasib (Diamond) wakati wa uzinduzi rasmi Studio za WASAFI FM Zanzibar 88.9 Desemba 13,2022 zilizopo Kilimani jijini Zanzibar, kulia ni Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi. (Picha na Ikulu). Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi Media,Abdul Nasib (Diamond) wakati wa uzinduzi rasmi Studio za WASAFI FM Zanzibar 88.9 Kilimani jijini Zanzibar, mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi Studio za WASAFI FM Zanzibar 88.9 katika Ofisi za Wasafi Media Kilimani jijini Zanzibar, wa pili kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi Media,Abdul Nasib (Diamond), Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi, Mhe,Idrisa Kitwana Mustafa(kushoto), Mke wa Rais Mama Mariam Mwinyi (wapili kulia) na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Mhe,Tabia Maulid Mwita. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (katikati) alipokuwa akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi Media,Abdul Nasib (Diamond) akiwa katika ofisi za Studio za WASAFI FM Zanzibar 88.9 katika uzinduzi rasmi wa Studio hizo uliofanyika Kilimani jijini Zanzibar wakiwemo na watangazji na waandishi wa habari. Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi Media,Abdul Nasib (Diamond) alipokuwa akizungumza na machache wakati wa uzinduzi rasmi Studio za WASAFI FM Zanzibar 88.9 katika Ofisi za Wasafi Media Kilimani jijini Zanzibar,uzinduzi uliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani). Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akizungumza na viongozi na wananchi wakati wa uzinduzi rasmi wa Studio za WASAFI FM Zanzibar 88.9 zilizopo Kilimani jijini Zanzibar.Baadhi ya Viongozi mbalimbali na waalikwa wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza nao wakati wa uzinduzi rasmi wa Studio za WASAFI FM Zanzibar 88.9 hafla iliyofanyika Kilimani jijini Zanzibar . Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt.Hussein Ali Mwinyi (kulia) alipokuwa akimkabidhi cheti cha Usajili wa Studio za WASAFI FM Zanzibar 88.9 Mkurugenzi Mkuu,Abdul Nasib (Diamond) wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Studio hizo zilizozinduliwa Kilimani jijini Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news