Rais Dkt.Samia atunukiwa tuzo ya muongoza watalii bora nchini

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan ametunukiwa tuzo ya muongoza watalii bora nchini kutoka Taasisi ya Kimataifa ya International Iconic Awards ya nchini India.

Tuzo hiyo imemtambuaMheshimiwa Rais Dkt.Samia kama muongoza wataliii bora kupitia filamu ya Tanzania The Royal Tour ambayo imetajwa kuleta ushawishi wa kitalii nchini.
Filamu hiyo iliyotengenezwa kuonesha vivutio vya utalii nchini ilizinduliwa hivi karibuni huku ikitajwa kuwa, itakuwa mkombozi wakati huu ambapo mataifa mbalimbali ikiwemo Tanzania yanahaha kujikwamua kiuchumi baada ya janga la ugonjwa wa UVIKO-19 ambao ulididimiza sekta nyingi ikiwemo ya utalii.

Tuzo hiyo imepokelewa Desemba 11, 2022 na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Pindi Chana kwa niaba ya Rais Dkt.Samia jijini Dodoma.

Waziri Dkt.Chana amesema, tuzo hiyo itaipa chachu Serikali kuendelea kuboresha miundombinu rafiki na kuweka bunifu mbalimbali kwenye sekta ya utalii.

Amesema,sekta ya utalii imeendelea kukuwa nchini kwani mwaka 2021 Tanzania ilipokea watalii 992,692, lakini mwaka 2022 imepokea watalii zaidi ya milioni moja huku wengine wakiendelea kuingia.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Juma Mkomi amesema Serikali inatoa fursa kwa wawekezaji kuja Tanzania kuwekeza kwenye sekta ya utalii kibiashara zaidi ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya vyuo vya utalii, hoteli, migahawa na viwanda mbalimbali nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news