Waziri Simbachawene:Vijana huu ni uzalendo mkubwa sana, Mungu awabariki

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene amepongeza vijana waliojiunga katika Kikundi cha Kisima umoja Vijana kwa moyo wao wa uzalendo wa kuchangia madawati katika shule ya Msingi Kisima.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene akimkabididhi Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisima madawati.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene katika ziara yake ya kutembelea na kuzungumza na wananchi katika Jimbo lake la uchaguzi Kibakwe lililopo Halmashauri ya Mpwapwa.
“Vijana wameweza kuchangia madawati 14 yenye thamani karibu ya milioni moja, ni jambo kubwa na vijana wengine igeni mfano wa vijana hawa.

"Wamekumbuka nyumbani, wameona wadogo zao wakae mahali pazuri kwa kuamua kutengeneza madawati, na umoja wao ni wa watu ambao hawana kitu, lakini ni umoja ambao unadhamira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akipokea madawati ya Kisima Umoja Vijana.

“Jambo la msingi katika maisha ni kuwa na dhamira na jambo lako, kwa sababu Mungu anabariki mipango, Mungu anabariki dhamira.

"Kwa niaba ya viongozi serikalini na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi naomba niwashukuru sana kwa tendo hili linaloonesha umoja ni nguvu,"amesema Mheshimiwa Waziri.

Akisoma taarifa ya Kikundi cha Kisima Umoja Vijana, mbele ya Waziri, Bw.Kepher Mdachi amesema, malengo yao ni kuendelea kusaidia jamii yao na ambazo ziko ndani ya uwezo wa kikundi hicho.

“Kutoa hamasa kwa wanafunzi ili kuongeza ufaulu, kutoa elimu kwa jamii kwa kuwafikia wazazi na walezi ili kuwahamasisha umuhimu wa elimu kwa vijana wao.”

Aidha, kikundi hicho kimelenga kujenga taasisi imara itakayolenga kusaidia jamii na kufanya jambo la kijamii kila mwisho wa mwaka ikiwa ni pamoja na kusaidia sekta ya afya kwa kuchangia vifaa tiba vyenye uhitaji wa haraka.
“Madawati haya yamepatikana kutokana na utaratibu wa kutoa ada kwa kila mmoja kuanzia shilingi 2,000 kadiri anavyojaliwa, na hufanywa kwa hiari. Tumezidi kuwa wamoja pale tunaposikia changamoto za kijamii ikiwa ni pamoja na kusaidiana sisi wenyewe kama mmoja wanakikundi amepata shida,”amesema Mdachi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news