Rais Hichilema afarijika kuona wananchi wanajinunulia mafahali Ranchi ya Taifa kwenda kuboresha mifugo yao

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Zambia,Mheshimiwa Hakainde Hichilema amesema anafarijika kuona wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini humo wanajitokeza kununua ng'ombe dume (mafahali) katika Ranchi ya Taifa Naminwe kwa ajili ya kwenda kuboresha mifugo yao.
Mheshimiwa Hichilema ameyasema hayo Desemba 30, 2022 baada ya kushuhudia mnada wa mafahali hao uliofanyika katika Ranchi ya Taifa Naminwe iliyopo Wilaya ya Namwala katika Mkoa wa Kusini mwa Zambia.

"Nilichukua muda kushuhudia mnada wa mafahali katika Ranchi yetu ya Naminwe huko Namwala. Inatia moyo kuona wananchi wenzetu kutoka kote Zambia wakija kwenye ranchi kununua mafahali kwa ajili ya kuboresha mifugo yao ambayo itawaletea mavuno bora,"ameeleza Rais Hichilema.
Picha zote kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Zambia kupitia https://twitter.com/HHichilema

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news