Saudi Arabia yawasilisha ombi la kuandaa fainali za Kombe la Asia la Wanawake 2026

NA DIRAMAKINI

SHIRIKISHO la Soka la Saudi Arabia (SAFF) limewasilisha rasmi ombi lake la kuandaa fainali za Kombe la Asia la Wanawake la 2026 la Shirikisho la Soka la Asia (AFC).

Mkurugenzi wa Shirikisho la Soka la Asia anayesimamia jalada la Kombe la Asia alikaribisha ujumbe wa Saudia katika makao makuu ya AFC yaliyopo jijini Kuala Lumpur,Malaysia.

Kocha msaidizi wa kwanza wa timu ya soka ya wanawake ya Saudia, Dona Rajab, mwanachama wa timu ya taifa ya Saudi Raghad Helmy, na mchezaji chipukizi Marya Baghaffar walikabidhi zabuni hiyo kwa shirikisho.

Yasser Al-Mishal, Rais wa Bodi ya Wakurugenzi ya SAFF alisema, kuandaa mashindano hayo kunafungua upeo mpya kwa soka la wanawake katika Ufalme na kanda.

"Ufalme una miundombinu imara ya michezo inayoiwezesha kuwa mwenyeji wa Kombe la Wanawake la Asia, kwani inakaribisha wageni kutoka Bara la Asia na duniani kote," alisema.

Al-Mishal alisema: "Tulijitayarisha tangu mapema kwa mashindano haya kulingana na viwango vya juu zaidi vya maandalizi, na faili la Saudi Arabia ni pana na limejaa maelezo ambayo yataboresha fainali za Kombe la Wanawake la Asia 2026."

Alieleza kuwa, Ufalme huo, kwa kuandaa fainali za Kombe la Wanawake la Asia 2026, unalenga kuliweka Shirikisho la Saudia katika nafasi muhimu ya kufanikisha soka la wanawake, katika hafla ya kimataifa ambayo inaweka Ufalme huo kwenye ramani ya kimataifa ya michezo.

Faili la Shirikisho la Soka la Saudi linajumuisha mahitaji, masharti na vigezo vya mashindano hayo, pamoja na matukio ya kimichezo ya kikanda na kimataifa ambayo Ufalme huo uliandaa kwa miaka michache iliyopita na umepata sifa duniani kote.

Saudi Arabia inashindana kuandaa michuano hiyo na Jordan, Australia na Uzbekistan, na Shirikisho la Soka la Asia linatarajiwa kufanya uamuzi wake na kutangaza nchi mwenyeji wa michuano hiyo mwaka 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news