Serikali yasisitiza ushirikiano mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa watoto

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu, Mhe. George Simbachawene ahimiza ushirikishwaji wa wadau wote katika kuunganisha nguvu ili kupambana na ukatili wa kijinsia kwa watoto.
Kauli hiyo ameitoa wakati akiongoza kikao kilichowakutanisha Mawaziri wa Kisekta kilichofanyika leo jijini Dar es salaam, kilicholenga kuimarisha mikakati ya kupambana dhidi ya ukatili wa kijinsia kwa watoto. 

Waziri Simbachawene amemuelekeza Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu kwa kushirikiana na wataalamu waandae miongozo yote izungumze kwa pamoja kuhusu ukatili wa kijinsia na baada ya kikao cha mawaziri ushauri upelekwe kwa Waziri Mkuu ili aridhie.

"Ili hatua za muda mfupi hatua za muda wa kati na hatua za muda mrefu ziweze kuchukuliwa katika kupambana na vita hii, binadamu wamekuwa waajabu kuliko wanyama matukio mengi ya ukatili wa kijinsia yanafanywa na ndugu wa karibu,"amesema.
Katika kikao hicho Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Mhe. Dkt. Doroth Gwajima amesema, mwaka 2021 viliripotiwa vitendo vya unyanyasaji wa watoto 11499.

“Uliongoza ni ukatili wa ubakaji 5899 na waliolawitiwa 1114 na waliopata mimba za utotoni ni 1677 na utafiti ukaonesha namba hizi uzigawe kwa 60, utaona asilimia 60 inafanyika nyumbani walipo baba na mama ndugu jamaa na marafiki na asilimia 40 ni nje ya nyumbani, wakiwa shuleni au wanapoenda shuleni.”

"Lazima tuimarishe mifumo izungumze na uwajibikaji, sheria tunazo tayari tuna miongozo mbalimbali sasa tunahitaji mawasiliano yaanzie kwa Mawaziri yashuke kwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, ishuke kwenye kata zetu, ishuke kwenye mitaa na vijiji.
“Mfumo wa mawasiliano uende kwenye kamati za mabaraza ya madiwani kwenye Halmashauri zetu, lakini kwenye vikao vya maendeleo vya kata ili viwe na nguvu ya kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto ili hata marekebisho ya sheria ndogo ndogo yaanzie kule chini,” alisema Waziri Gwajima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news