Ujerumani yashindwa kufuzu kwa hatua ya mtoano kwa mara ya pili mfululizo katika Kombe la Dunia

NA DIRAMAKINI

LICHA ya Ujerumani kuishinda Costa Rica kwa mabao 4-2 katika mechi ya kusisimua, lakini mabingwa hao mara nne wameshindwa kutinga hatua ya makundi kupitia michuano ya Kombe la Dunia kwa mara ya pili mfululizo.

Mwaka 2018, Ujerumani walinyooshwa na Korea Kusini kupitia mabao ya Kim Young-gwon dakika ya 92 na Son Heung dakika ya 96 kupitia hatua kama hiyo,michuano ya Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) iliyochezwa katika dimba la Kazan Arena nchini Urusi.

Aidha,Japan imeishangaza Uhispania katika mechi nyingine ya Kundi E na kumaliza kileleni mwa kundi hilo wakiwa juu huku Uhispania ikishika nafasi ya pili baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1.
Kila mmoja anapambana kuhakikisha ushindi unapatikana kwa Taifa lake. (Picha na Showkat Shafi/Al Jazeera).

Ujerumani ilimenyana na Costa Rica, Desemba 1, 2022 katika dimba la Al-Bayt lililopo Al Khor nchini Qatar kupitia michuano ya Kombe la Dunia ya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) inayoendelea.

Mabao kutoka kwa Serge Gnabry dakika ya 10, mabao mawili ya Kai Hervertz dakika ya 73 na 85 na bao lingine la Niclas Fullkrug dakika ya 89 hayakutosha kwa mabingwa hao wa 2014, ambao walihitaji kuzidi tofauti ya mabao ya Uhispania ili kupata nafasi.

Costa Rica waliibuka zikiwa zimesalia dakika 20 kabla ya bao la kusawazisha kutoka kwa Yeltsin Tejeda dakika ya 58, na Juan Pablo Vargas dakika 70. Costa Rica wangeweza kufuzu pamoja na Japan kwa ushindi, lakini mambo yakawaendea kombo.

Japan itamenyana na Croatia katika raundi inayofuata, huku Uhispania ambayo imefuzu kama mshindi wa pili itacheza dhidi ya Morocco.

Ujerumani, licha ya kuambulia alama sawa na Uhispania, iliondolewa kwa sababu ya tofauti ya mabao kati ya pande hizo mbili.

Aidha, maswali sasa yanaelekezwa kwa kocha wa Ujerumani, Hansi Flick ambaye aliwaambia waandishi wa habari kwamba atasalia kama bosi wa timu hata kama watashindwa kufuzu kwa raundi inayofuata, Je? Atasalia, muda utasema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news