Spika Dkt.Tulia atoa rai kwa wabunge wa Bunge la EAC kuhusu michezo

NA DIRAMAKINI

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson amewaasa Wabunge wa Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kudumisha kauli mbiu ya Mashindano ya kila mwaka ya kimichezo ya Mabunge hayo ambayo ni 'Kupanua na Kuimarisha Muungano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki'.
Akizungumza Desemba Mosi, 2022 wakati wa hafla ya ufungaji wa Mashindano ya 12 ya michezo hiyo jijini Juba nchini Sudan Kusini, Dkt.Tulia amesema ni lazima kauli mbiu ya mashindano hayo iendelee kudumishwa ili iweze kuleta matokeo chanya katika kusaidia Jumuiya ya Afrika Mashariki kuendelea kuwa na umoja.

"Kauli mbiu ya Mashindano haya lazima iendelee kudumishwa, hatujaja kushidana bali kujenga umoja wa Jumuiya yetu," amesisitiza Spika Dkt.Tulia.

Ameongeza kuwa, kuwepo kwa rufaa nyingi baina ya timu na timu katika mashindano hayo kunaonesha kwamba kuna tatizo.
"Tunapoona rufaa nyingi inaashiria kuna tatizo na hivyo ni lazima tubadilike hatuwezi kushiriki Mashindano haya wakati tunaendelea kudanganyana," amesema Dkt.Tulia Ackson.

Mbali na hayo, Dkt. Tulia alisititiza pia kwamba lazima sheria za Mashindano hayo ziheshimiwe ili kusonga mbele.

"Mashindano haya si Kombe la Dunia ni kwa ajili ya kujuana na kudumisha umoja wetu," alisema Dkt. Tulia na kuongeza kwamba; kwa rufaa na udanganyifu unaojitokeza wakati wa Mashindano hayo, malengo ya kujenga jumuiya imara hayawezi kufikiwa.
Kwa upande mwingine, Spika Dkt Tulia aliishukuru Sudan Kusini kwa kuandaa Mashindano hayo na kipekee kuipongeza kwa kufanya vizuri ingawa ni nchi changa na ngeni.

"Tutatangaza tulichoona mnafanya vizuri, hongereni sana," alisema. Spika Dkt. Tulia aliongeza pia Sudan Kusini kwa jinsi walivyohamasisha wananchi kufika viwanjani kushuhudia mashindano hayo.
"Mashindano haya si kwa ajili ya Wabunge tu, ni kwa ajili ya wananchi hivyo nawapongeza Sudan Kusini kwa sababu wanachi walijitokeza kwa wingi kushuhuhudia Mashindano haya," amesema.

Spika Dkt. Tulia amehitimisha kwa kuwaambia washiriki wa Mashindano hayo kurudi katika nchi zao na ujumbe kwamba Sudan Kusini kuna amani tele tofauti na jinsi ambavyo imekuwa ikisikika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news