VIFAFIO yapata Bodi ya Wadhamini

NA DIRAMAKINI

SHIRIKA lisilokuwa la kiserikali la Victoria Farming and Fishing Organization (VIFAFIO) linalojishughulisha na kuhudumia wakulima, wafugaji na wavuvi lenye makao makuu yake katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara limepata bodi ya wadhamini wataohudumu kwa kipindi cha miaka mitatu.
Wajumbe hao wamepatikana kupitia wanachama wa mkutano mkuu wa shirika hilo uliofanyika Desemba 21, 2022 katika ofisi za shirika hilo Mjini Musoma chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake, ndugu Costantine Nyeriga.

Wajumbe hao wamepongeza juhudi za Meneja wa Shirika hilo, Majura Maingu anazozifanya ikiwemo kuhakikisha shirika hilo linaendelea kuhudumia vikundi vya wakulima, wafugaji na wavuvi.
Kwa upande wake Meneja wa Shirika hilo la VIFAFIO amewaeleza wanachama wa mkutano mkuu huo kuwa Shirika hilo kwa ufadhili wa Foundation for Civil society linatekeleza Mradi wa "Funguka kutokomeza vitendo vya ukatili wa Kijinsia uliozoeleka katika maeneo ya Uvuvi" katika kata Saba za Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na kata Nne katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani humo.

Maingu amesema, shirika hilo pia litatekeleza mradi wa Uhifadhi na Uvuvi endelevu eneo Oevu la mto Mara kwa ufadhili wa Shirika la WWF.

Maingu amesema, mradi huo utalenga kuboresha utunzaji wa mazingira hasa maeneo ya mazalia ya samaki katika Mto Mara na Ziwa Victoria.
Mkutano huo pia umewachagua wajumbe wanachama wawili ili kukamilisha idadi ya wajumbe wa bodi wa shirika hilo.

Waliochaguliwa ni Tendo Makori kutoka Wilaya ya Butiama na Godliver Mfungo kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.

Akiongea katika Mkutano huo mjumbe mpya wa Bodi Tendo Makori amewasihi watendaji wa shirika hilo kusimamia miradi hiyo inayotekelezwa kwa ufadhili wa wabia kwa weledi mkubwa.

Kwa upande wake Boazi Nyeura amewasihi wanachama wa shirika hilo kuendeleza mshikamano katika kuendeleza shirika kwa kujitolea.

Pia, Boaz amemuomba Meneja wa shirika hilo kuendelea kubuni miradi na kuhamasisha wanachama wengi kujiunga na shirika la VIFAFIO.
Katibu wa Shirika hilo, Steven Mandago amewataka wanachama wa shirika hilo, kujitolea katika kuimarisha hali ya shirika ili jamii inufaike zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news