Mchina akamatwa kwa kuingilia mfumo wa mawasiliano Tanzania

NA DIRAMAKINI

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemkamata LI NAIYONG (48) raia wa China, ambaye anatuhumiwa kujihusisha na shughuli za kuingilia mfumo wa mawasiliano kinyume na taratibu za nchi.Hali hiyo imetajwa kuisababishia Serikali hasara ya kiasi cha shilingi milioni 221,163,600.

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa na Kamanda Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam,ACP Muliro J. Muliro ambapo mafanikio hayo yanatokana na ufuatiliaji mkali unaoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi na timu hiyo maalum.

Amesema, mtuhumiwa huyo amekuwa akituma vifaa visivyo rasmi kuwaunganisha watu kwa simu kufanya mawasiliano nje ya nchi kinyume na sheria za mmlaka ya mawasiliano Tanzania.

"Jeshi la Polisi halitasita kuchukua hatua kali kwa mtu au watu wote watakaovunja sheria, kanuni na miongozo inayoelekeza matumizi sahihi ya mitandao,"amefafanua Kamanda ACP Muliro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news