WANAFUNZI MILIONI 1.74 KUANZA KIDATO CHA KWANZA KWA AWAMU MOJA 2023

NA OR-TAMISEMI

NAIBU KATIBU Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu, Dkt. Charles Msonde amesema wanafunzi 1,073,941 waliochaguliwa kidato cha kwanza 2023 wataanza shule kwa wakati mmoja.

Hatua hiyo inafanya kusiwepo na utaratibu wa chaguo la pili (second selection) kama ilivyozoelekea kutokana na kukamilika kwa madarasa 8,000.

Dkt. Msonde ameyasema hayo wilayani Kongwa mkoani Dodoma wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa.

Amesema, hakutakuwa na changuo la pili kwa wanafunzi wanaotarajia kujiunga na kidato cha kwanza Januari 2023 na kuwasihi wazazi na walezi kuhakikisha wanafunzi wote waliochaguliwa wanaripoti shuleni kwa wakati.

"Kwa mwaka 2023 hakutakuwa na second selection (chaguo la pili la wanafunzi) kwa sababu fedha zilizotolewa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika sekta ya elimu zimetosha kuboresha miundombinu ya kuwachukua watoto wetu wote kwa intake (mkupuo) mmoja."

Amesema, tangu Rais aingie madarakani ameshatoa fedha zilizowezesha kujenga zaidi ya vyumba vya madarasa 20,000 ndani ya miaka miwili hatua ambayo imewaondolea adha watoto kwa kuanza masono kwa pamoja huku wazazi wakiwa hawajachangishwa kitu.

Katika kukabiliana na ongezeko la wanafunzi kwa mwaka 2023, Rais Dkt. Samia ametoa shilingi bilioni 160 zilizotumika kujenga madarasa 8,000.

Dkt.Msonde amesema,ujenzi wa madarasa hayo nchi nzima umekamilika kwa asilimia 95.6 na yaliyobakia wako kwenye hatua za ukamilishaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news