WANAHABARI WAOMBEWA KUWA WAKWELI

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wamewaombea Waandishi na Watangazaji wa Habari wafanye kazi zao vizuri, maombi hayo yamefanyika leo Desemba 4, 2022 katika misa ya Jumapili ya pili ya Majilio ya Mwaka A wa kanisa katika Kanisa la Bikira Maria Imakulata, Parokia ya Chamwino Ikulu, Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma.
“Uwasaidie Waandishi na Watangazaji wa Habari waseme ukweli na kuzingatia maadili ya kazi zao Ee Bwana, Twakuomba utusikie.”

Maombi haya yalikuwa ya pili katika mlolongo wa maombi matano ya misa hii iliyoisalishwa parokiani hapo ikiongozwa na Padri Paul Mapalala, Paroko wa Parokia hiyo, akihubiri katika misa hiyo amesema katika kipindi cha majilio Wakristo wanaandaliwa kwa ajili ya kuzaliwa mwokozi huku nyakati hizo zinapita mara nyingi kila mmoja kwa umri wake.

“Wengine Wakristo wa siku nyingi, wengine wa miaka michache na tunamchukuliaje huyo Kristo katika mazingira yetu? Tunampelekaje katika mazingira yetu?.

"Tunaugeuzaje ulimwengu wetu, ndiyo maana ya haya , vipindi hivyo vya kanisa vinajirudia sana katika maisha yetu, inategenea na umri utakavyoishi, wa umri mkubwa ndiyo vitakujia mara nyingi sana, je vinakuandaaje?.

"Vinakutayarishaje kumsogelea Mungu? Kumkaribia Kristo na kuwa Mkristo bora na kuwa mwalimu wa wengine kama mitume walivyokuwa?".

Misa hiyo ilisaliwa katika hali ya utulivu mkubwa huku upepo ukivuma kwa kadiri ukigonga kuta na na paa za kanisa hili lililopo katika eneo la mwiinuko.

Mpaka Padri Paul Mapalala anahitimisha misa ya kwanza ya Jumapili ya pili ya majilio kanisani hapa eneo la Chamwino Ikulu halikujaliwa kupata mvua wala manyunyu kwa juma zima huku anga likiendelea kuwa na mawingu kiasi ambayo yameendelea kuwatia moyo wakulima wa eneo hili, kwani bado wanaendelea kufukia mbegu ardhini katika mashamba yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news