Wanasheria,Waendesha Mashtaka na Wapelelezi chini ya Wizara ya Maliasili wanolewa

NA JOHN BERA

WIZARA ya Maliasili na Utalii kupitia Kitengo cha Huduma za Sheria imeendesha mafunzo kwa Wanasheria,Waendesha Mashtaka na Wapelelezi walioko chini ya wizara hiyo ili kuwajengea uwezo kuhusu Sheria za kisekta na Sheria Mtambuka kwa lengo la kupunguza matukio ya ujangili wa mazao ya misitu na wanyamapori kwenye maeneo yaliyohifadhiwa.
Baadhi ya Wanasheria,Waendesha mashtaka na wapelelezi walioko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Mahakimu wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa na Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Maliasili na Utali, Lucy E, Salekoi kwenye Mafunzo ya Wataalamu hao yanayofanyika jijini Mwanza.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo jijini Mwanza, Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Bi. Lucy Saleko amesema kuwa mafunzo hayo yameandaliwa na Kitengo cha Sheria chini ya udhamini wa Mradi wa Kuzuia na Kupambana na ujangili wa wanyamapori na Biashara haramu ya nyara na mazao ya misitu (CPIWT Project), UNDP na Global Environmental Facility (GEF) chini ya ufadhili wa Benki ya Dunia.
Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Lucy E Saleko akizungumza kabla ya kuanza kwa Mafunzo kwa Wanasheria,Waendesha mashtaka na wapelelezi walioko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Mwanza.

“Sisi kama kitengo cha Sheria ambao ndio waratibu wakuu wa mafunzo haya tumekuwa tukipata changamoto hususan kwenye makosa ya ujangili na mifugo kukamatwa kutokana na watu kuingiza hifadhini, mafunzo haya ni muhimu pale mashauri yanapopelekwa mahakamani kuhakikisha ushahidi unatolewa wa mtu aliyeingiza mifugo hifadhini haukwami", amesisitiza Lucy Saleko.
Amesema, kutokana mafunzo hayo,Wanasheria,Waendesha mashtaka na wapelelezi walioko chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii wataongeza ujuzi katika kudhibitisha vielelezo vya ushahidi na kukusanya taarifa za ushahidi wawapo mahakamani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news