Wauguzi Zanzibar wampa saluti Rais Dkt.Mwinyi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akihutubia wakati wa sherehe za kupongezwa zilizoandaliwa na Wauguzi wa Zanzibar kwa kutimiza miaka miwili ya uongozi wake, zilizofanyika leo Desemba 20,2022 katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Unguja jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu). Wauguzi Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani) wakati wa sherehe za kumpongeza kwa kutimiza miaka miwili ya uongozi zilizofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Unguja jijini Zanzibar leo.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza, Bi.Rabia Mzee Mataka wa Kitengo cha Shirikishi cha Afya na Uzazi Zanzibar, wakati akitembelea maonesho ya sherehe ya kumpongeza kwa kutimiza miaka miwili ya uongozi wake, iliyoandaliwa na Wauguzi Zanzibar,katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Wilaya ya Mjini Unguja na (kulia kwa Rais) ni Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Ahmed Nassor Mazrui na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja, Mhe.Rashid Simai Msaraka. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Tuzo Maalum ya Kutimiza Miaka Miwili ya Uongozi wake,iliyotolewa na Wauguzi Zanzibar, akikabidhiwa na Muunguzi Bi. Maryam Rashid Suleiman, wakati wa sherehe za kumpongeza zilizofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Unguja leo, na kulia kwa Muunguzi ni Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe.Nassor Ahmed Mazrui na kushoto kwa Rais ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja, Mhe.Rashid Simai Msaraka. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi akikata keki maalum ya kumpongeza kwa kutimiza miaka miwili ya uongozi wake, wakati wa sherehe za kumpongeza zilizoandaliwa na Wauguzi Zanzibar katika ukumbi wa Chuo cha Utalii Maruhubi Unguja jijini Zanzibar leo, na kulia kwa Rais ni Muunguzi Bi. Maimuna Ibrahim, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na Naibu Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Hassan K. Hafidh na kushoto kwa Rais ni Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Mhe. Rashid Simai Msaraka na Mwenyekiti wa Baraza la Wauguzi Zanzibar, Prof. Amina Abdulkadir Ali.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news