Wizara ya Afya yaifunga Ofisi ya Uratibu wa Mradi wa Ukimwi, TB na Malaria

NA MWANDISHI WETU

MENEJIMENTI ya Wizara ya Afya chini ya Katibu Mkuu,Prof. Abel Makubi imechukua hatua za kuifunga Ofisi ya Uratibu wa Mradi wa Ukimwi, TB na Malaria (COAg) iliyopo chini ya Wizara ya Afya ambayo inasimamiwa na Dkt. Peter Mgosha kwa kukaidi agizo la Rais na Waziri Mkuu kuhamia makao makuu Dodoma.
Prof. Makubi amebainisha hayo Jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Dkt. Mgosha amekaidi zaidi ya mara tatu agizo la kuhamia Dodoma pamoja na kukumbushwa na Menejimenti ya Wizara.

Katibu Mkuu ameagiza watumishi wote wa ofisi hiyo wafike Dodoma Jumatatu bila kukosa.
Menejimenti imechukua hatua ya kufunga ofisi hiyo na hatua zingine za kinidhamu ziendelee chini ya usimamizi wa Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news