Buriani Papa Benedict XVI

NA ADELADIUS MAKWEGA

“Mtumishi wa umma wa ngazi ya kati, Mkatoliki,hajaoa, mwenye umri wa miaka 43, mtu mwema, raia, anatafuta mwanamke wa kuoa, awe Mkatoliki, mwanamke mwaminifu.
 
"Awe anajua kupika, awe anaweza kuzifanya kazi zote za nyumbani kikamilifu, awe na ujuzi wa kushona nguo, awe ma malengo ya kuolewa, awe na matamanio, lakini siyo kabla ya ndoa.”
Papa Benedict XVI wakati wa uhai wake kabla ya kustaafu akiwabariki waumini wakati wa misa huko Islinger Feld Regensburg. (Picha na Arturo Mari/dpa).

Haya yalikuwa maelezo ya jarida la kila wiki la Kanisa Katoliki la Liebfraubote juu ya askari polisi aliyekuwa akisaka mchumba wa kuoa.

Maria Peintner, mwanamke wa Kijerumani, mwenye miaka 36, binti wa muoka mikate aliyesomea upishi alichangamkia fursa hiyo na baada ya miezi minne mwaka 1920 walioana na mwanaume aliyenadi hayo.
Joseph na Maria Ratzinger 

Katika ndoa yao Maria na Joseph walizaa watoto watatu Maria (1921), Georg (1924) na Joseph (1927). Huku jina la mtoto wa kwanza na jina la mtoto wa mwisho yakiwa majina ya wazazi hao.

Huyu mtoto wa mwisho Joseph ndiye Papa Mtakatifu Benedict wa XVI ambaye jina lake halisi ni Joseph Alois Ratzinger aliyefariki dunia Desemba 31, 2022 huko Vatican ambapo katika uhai wake aliwahi kushika nafasi kadhaa kubwa katika Kanisa Katoliki Ulimwenguni kama vile Askofu wa Roma na Mkuu wa Kanisa Katoliki Ulimwenguni tangu mwaka 2005-2013 alipojiuzulu nyadhifa hizo.

Akiwa Papa Mtakaffu alijiuzulu kama ilivyokuwa kwa Papa Mtakafifu Gregori XII mwaka 1415 miaka zaidi ya 600 iliyopita.
Kadinali Joseph Ratzinger akiwa na wazazi wake.

Mara baada ya kufariki dunia kiongozi huyu aliyewahi kuliongoza kanisa hilo lenye waumini zaidi ya bilioni moja Ulimwenguni anakumbukwa kwa mambo mengi.

Mojawapo ni kisa hiki kilichosimulia baada ya Papa Mtakatifu Benedict XVI enzi ya uhai wake mwaka 2006 alipotembelea eneo la Bavaria Kijiji cha Marktl am Inn Ujerumani alipokwenda kuzuru makaburi ya wazazi wake. 

Alishangazwa baada ya kubaini kuwa baba na mama yake yaani Joseph na Maria Ratzinger walikutana kwa mara ya kwanza katika tangazo la kutafuta wachumba ambapo Joseph Ratzinger alipojitangaza katika jarida la kila wiki la Kanisa Katoliki la Liebfraubote mwaka 1920. Ikiwa ni miaka 86 baada ya tukio hilo.

Maria Peintner mama wa Baba Mtakatifu Benedict wa XVI alipoona tangazo hilo alichangamkia fursa na kuolewa na afande Joseph Ratzinger, mama huyu hakuyafahamu ya kesho kuwa atazaa mtoto wake wa mwisho ambaye atakuja kuwa Baba Mtakatifu.

Hayo ndiyo maisha yalivyo, hakuna anayeifahamu kesho.Je msomaji wangu unafahamu wazazi wako kipi kiliwakutanisha?

Wakati Vatican inamzika Baba Mtakatifu Benedict wa XVI ,mimi na wewe tutafakari hilo la ndoa hiyo ndani yake aliyepozaliwa kiongozi huyu.
 
Wazazi wako walikutana wapi? Wewe na mumeo mmekutana wapi kwa mara ya kwanza?. Mwanakwetu anasema BURIANI BENEDICTI XVI.

0717649257

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news