Chama ndiye mchezaji bora wa mashabiki Desemba 2022

NA DIRAMAKINI

KIUNGO mshambuliaji wa Simba SC, Clatous Chama amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Desemba (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).

Chama amewashinda Nahodha John Bocco na mlinzi Shomari Kapombe ambao alikuwa ameingia nao fainali kwenye kinyang’anyiro hicho.

Katika mwezi Desemba 2022, Chama alicheza dakika 540 akifunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa mengine saba.

Mchanganuo wa kura ulivyokuwa

                        Kura            Asilimia

Chama             1829            54.52

Bocco               1415            42.18

Kapombe           111              3.31


Kwa kuibuka mshindi Chama atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.

Post a Comment

0 Comments