Fountain Gate yachezea kichapo kutoka Simba Queens

NA DIRAMAKINI

SIMBA Queens imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier League.

Ni kupitia mtanange uliopigwa Januari 4, 2023 katika dimba la Uhuru lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salam.

Fountain Gate walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 15 kupitia kwa Ritticia Nabbosa kwa kichwa baada ya walinzi wa Simba Queens kuonekana kuzembea kuokoa mpira wa kona.

Aidha, Kocha Charles Lukula alifanya mabadiliko ya mapema dakika ya 20 ya kumtoa mlinzi wa kati Daniela Mgoyi na kumuingiza Esther Mayala.

Nahodha Opa Clement awasawazishia Simba Queens bao hilo kwa mkwaju wa penati dakika ya 31 baada ya Jentrix Shikangwa kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Asha Djafar aliweka kambani bao la pili dakika ya 61 kwa shuti kali ndani ya 18 baada ya kutengwa na Opa mpira wa krosi uliopigwa na Shikangwa.

Pia kipindi cha pili Kocha Lukula aliwatoa Diana Mnali na Pambani Kuzoya na kuwaingiza Aisha Juma na Amina Ramadhani.

Ushindi hu unawafanya Simba Queenss kufikisha alama saba baada ya kucheza mechi nne, wakishinda mbili, sare moja na kupoteza moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news