JAJI MGEYEKWA AWAITA WANANCHI KUJIFUNZA USULUHISHI MIGOGORO YA ARDHI

NA MWANDISHI WETU

KATIKA kuadhimisha Wiki ya Sheria, Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi imeandaa siku moja ya kutoa elimu na kukutana na wadaawa katika viwanja vya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam siku ya Alhamisi ya Januari, 26, 2023.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi, Mhe. Agnes Mgeyekwa amesema siku hiyo Majaji wa Mahakama yake watakuwepo katika viwanja hivyo kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi.

Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kujifunza faida za usuluhishi katika masuala mazima ya utatuzi wa migogoro ya ardhi.

Kwa mujibu wa Mgeyekwa, Majaji wa Mahakama hiyo watakuwemo katika Banda hilo la Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi kuanzia saa 3 asubuhi hadi 9 alasiri ambapo watatoa elimu na kukutana na wadaawa.

"Ninawaomba wananchi wajitokeze kwa ajili ya kujifunza faida za usuluhishi katika utatuzi wa migogoro ya ardhi,"amesema Jaji Mgeyekwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news