Jela miaka 30 kwa kumbaka mtoto

NA DIRAMAKINI

MAHAKAMA ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara imemhukumu, Richard Martin (42) mkazi wa Kiijiji cha Minjingu kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 11 jina linahifadhiwa.

Hukumu hiyo imetolewa Januari 5,2023 mbele ya Hakimu Victor Kimario wa Mahakama ya Wilaya ya Babati ambapo mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Julai 2, 2022 huko katika Kijiji cha Minjingu jirani na Ziwa Manyara.

Imeelezwa Mahakamani hapo kuwa, mshtakiwa alimkuta mtoto huyo akiwa na kaka yake mwenye umri wa miaka 14 wakichunga ng'ombe ndipo akaomba kusaidiwa kwenda kupakiza gunia la mkaa, mtoto huyo na kaka yake walikubali kwenda kumsaidia, lakini baada ya kufika njiani mshtakiwa alimwambia kaka wa binti kwamba arudi kuangalia mifugo isipotee ndipo akaondoka na binti huyo kwenda kumbaka.

Majibu ya uchunguzi wa daktari baada ya kumpima mtoto huyo yalithibitisha kufanyiwa kitendo hicho huku akiwa na maumivu makali ambapo walimpatia dawa ya kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi.

Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Grace Mgaya ameiomba Mahakama itoe adhabu kali ili iwe fundisho kwa mshtakiwa pamoja na wengine wenye tabia kama hiyo huku mshtakiwa akiiomba Mahakama impunguzie adhabu kwani ana watoto watatu ambao ni wadogo na mama yao alishafariki hivyo wanamtegemea wakiwemo wazazi wake.

..nilikuwa natembea nikakutana na binti wa miaka kati ya 10 na 11 akiwa na wenzake wanachunga ng'ombe, nikaongea nae nikamwambia nataka penzi lako ambapo alikubali nikamuingizia na kummwagia shahawa mara moja..."

Wakati huo huo, Hakimu Kimario amesema, mshtakiwa anayo haki ya kukata rufaa ndani ya siku 30 kuanzia siku ya hukumu hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news