JKT Queens yawaburuza vigogo wa soka nchini

NA DIRAMAKINI

JKT Queens imeendelea kushikilia nafasi ya kwanza katika Msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite (SWPL).

Ni baada ya raundi ya tano kutamatika ambapo, JKT Queens imejikusanyia alama 13 bada ya mechi tano huku nafasi ya pili ikishikiliwa na Fountain Gate Princess kwa alama 12 baada ya mechi tano.

Katika ligi hiyo ambayo inaundwa na timu 10, nafasi ya tatu katika msimamo huo inashikiliwa na Yanga Princess ambayo baada ya mechi tano imejikusanyia alama 10 huku nafasi ya nne ikishikiliwa na Simba Queens kwa alama 10 baada ya mechi tano.

Wakati huo huo, nafasi ya tano inashikiliwa na Alliance Girls kwa alama saba baada ya mechi tano huku Mkwawa Queens ikiburuza mkia kwa alama moja baada ya mechi tano. Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),michezo ya raundi ya sita inachezwa kesho, huku swali kuu likiwa JKT Queens wataendelea kukaa kileleni?.

Post a Comment

0 Comments