Ni Singida Big Stars au Kagera Sugar FC leo?

NA DIRAMAKINI

LEO Januari 17, 2023 michuano ya Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara itaendelea kwa miamba wawili wa soka kuumana.

Miamba hao ni Singida Big Stars FC kutoka mkoani Singida ambao wataumana na Kagera Sugar FC kutoka mkoani Kagera.

Mtanange huo utapigwa majira ya saa 10 jioni katika dimba la Liti lililopo mkoani Singida, ambapo wawili hao wanakutana huku Singida Big Stars ikiwa nafasi ya nne kwa alama 37.
 
Ni baada ya mechi 19 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara ambayo inaundwa na timu 16.

Aidha, Kagera Sugar FC inashika nafasi ya nane ikiwa na alama 24 baada ya mechi 19. Hivyo, ushindi wa leo utamuongezea mmoja wapo alama muhimu katika ligi hiyo yenye ushindani na mvuto mkubwa nchini.

Post a Comment

0 Comments