Kocha Lukula afunguka kuhusu ushindi wa Simba Queens

NA DIRAMAKINI

KOCHA Mkuu wa Simba Queens, Charles Lukula amesema mabadiliko aliyofanya ya wachezaji wawili yaliifanya timu hiyo kuongeza kasi kutoka nyuma na kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fountain Gate.

Ni kupitia mtanange uliopigwa Januari 4, 2023 katika dimba la Uhuru lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salam.

Amesema, ilibidi amtoe Daniela Mgoyi mapema kipindi cha kwanza na kumuingiza Esther Mayala ambaye aliituliza safu ya ulinzi kabla ya kufanya hivyo kwa Diana Mnali kipindi cha pili na kumuingiza Aisha Juma na kuifanya timu kuwa na uwiano mzuri wa kuzuia na kushambulia.

Kocha Lukula aliwasifu wachezaji kwa utulivu waliokuwa nao ambapo licha ya kuwa nyuma kwa bao moja hawakutetereka na kupambana mpaka kufanikiwa kupata alama tatu.

“Mchezo ulikuwa mgumu Fountain ni timu nzuri na imejipanga vizuri, nawapongeza wachezaji wangu kwa kazi kubwa waliyofanya na kusaidia kupatikana kwa alama tatu.

“Ligi ya msimu huu ni ngumu kila timu imejipanga, mchezo dhidi ya Fountain imeisha tunajipanga kwa mechi ijayo,” amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news