Kocha Mkuu Simba SC ahitaji mshambuliaji mpya mwenye nguvu

NA DIRAMAKINI

BAADA ya Kikosi cha Simba kufanya mazoezi na kikosi kwa siku mbili katika kambi waliyoweka nchini Dubai, Kocha Mkuu Oliveira Roberto ‘Robertinho’ amejiridhisha kuwa anahitaji mshambuliaji mwingine.
Robertinho amesema, kikosi chake kina washambuliaji wazuri huku akimwagia sifa Nahodha John Bocco, lakini ameweka wazi kuwa ili atimize malengo yake anahitaji mshambuliaji mwingine wa kusaidiana na waliopo.

“Aina ya mshambuliaji ninayemtaka ni mwenye nguvu, kasi na maarifa ya kufunga,”amesema Roberthinho baada ya kumaliza mazoezi.

Hiyo ilikuwa ni siku ya pili kikosi hicho kikiendelea na mazoezi mjini Dubai ambapo awali walifanya mazoezi mara moja na kuanzia leo timu itafanya mazoezi mara mbili yaani asubuhi na jioni.

Kocha Robertinho anasema, ameamua kuongeza muda wa mazoezi ili kupandisha nguvu ya timu pamoja na utimamu wa mwili.

Aidha, kw amujibu wa taarifa kutoka klabu hiyo, kwa sasa klabu ipo kwenye mawindo ya kutafuta mshambuliaji ili kuongeza ubora kwenye eneo hilo ambapo kabla dirisha dogo halijafungwa mshambualiaji mpya atatangazwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news