Mama Mariam Mwinyi awamegea wana michezo siri ya mafanikio

NA DIRAMAKINI

MKE wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi amewataka wana michezo kutoridhika na viwango walivyofikia, waongeze bidii ili kuwa na viwango vya umahiri.
Mchezaji wa Timu ya Zimamoto, Pendo Adrian Mpela akiwa na mpira wakati wa mchezo wao wa Ufunguzi wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi na Timu ya KVZ,uliofanyika katika uwanja wa Gmykhana, Timu ya KVZ ilishinda mchezo huo kwa mabao 44 -41.(Picha na Ikulu).

Ameyasema hayo Januari 4, 2023 wakati wa uzinduzi wa michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa mpira wa netiboli huko Gymkhana jijini Zanzibar.

Mama Mariam Mwinyi amesema, anajua kwamba michezo ni afya, burudani, urafiki, nidhamu lakini katika Dunia wanayoishi sasa michezo ni ajira yenye malipo na ujira mkubwa.

"Sote ni mashahidi, tunasoma, tunasikia, tunajionea namna wanamichezo mbalimbali waliofikia viwango vikubwa wanavyolipwa mamilioni ya fedha na wachezaji mahiri. Leo hii duniani ni matajiri wakubwa na mabilionea kutokana na ujira mkubwa wanaolipwa,"amesema.
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mama Mariam Mwinyi akirusha mpira golini kuashiria kuyafungua Mashindano ya Kombe la Mapinduzi katika Uwanja wa Gmkhana Wilaya ya Mjini Unguja.

Pia amewataka kujiuliza wao kama wana michezo wanakwama wapi kufikia viwango hivyo na kusema kwamba huenda baadhi yao hawajawa na dhamira ya kweli ya kutambua kuwa michezo ni ajira.

Hata hivyo amesema ni wajibu wa jamii ya wanamichezo wote nchini kutafakari kuweka malengo na kuamua kwenda kwenye viwango vya juu zaidi vya kimataifa.
"Tufikie pahali nchi yetu iwe na wanamichezo wanaowika katika majukwaa ya kimataifa kwa fani zote, tujiulize wale waliofikia huko wana nini na kwa namna gani, kinachohitajika hapa, ni nia, malengo na jitihada na ninaamini kabisa uwezo munao,"amesema Mama Mariam Mwinyi.
Sambamba na hayo amesema, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa umuhimu mkubwa katika sekta ya michezo nchini na kwa kutihibitisha hilo imeunda wizara ya kushughulikia michezo ili kuongeza kasi ya ukuaji wa sekta hiyo.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fatma Hamad Rajab amesema, lengo la mashindano hayo pamoja na kuwa wanaibuwa vipaji, lakini pia wanaunga mkono juhudi za Serikali za kuimarisha na kukuza michezo nchini.
Rajab amesema, mashindano hayo yameandaliwa kuungana na wananchi wote kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ambayo kilele chake ni Januari 12, mwaka huu.

Awali Katibu Mkuu wa Chama Cha Netiboli Zanzibar (CHANEZA), Said Ali Mansab alisema mashindano hayo ni kiunganishi baina ya wachezaji na viongozi katika kupeleka mbele gurudumu la michezo Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news