MANDONGA KIMATAIFA

NA LWAGA MWAMBANDE

USIKU wa kuamkia Januari 15, 2023 Bondia Mtanzania Karim Mandonga (Mtu Kazi) amemtandika Mkenya, Daniel Wanyonyi katika pambano la raundi 10.

Picha na The Star.

Ni katika ukumbi wa Tsavo Ballroom KICC jijini Nairobi ambapo Mandonga aliibuka mshindi baada ya Wanyonyi kukubali kushindwa raundi ya sita katika pambano hilo.

Baada ya kutembeza kichapo hicho, Mandonga ameahidi kurejea tena nchini Kenya ifikapo Aprili, mwaka huu kwa ajili ya kwenda kumchakaza mtu. Mshairi wa kisasa, Lwaga Mwambande anasema, kila penye nia na bidii kuna mafanikio. Endelea;

1:Mandonga kimataifa,
Umetuletea sifa,
Mtu alitaka kufa,
Hongera sana Mandonga.

2:Mtu kazi maarifa,
Wala wewe siyo lofa,
Tukuandalie dhifa,
Hongera sana Mandonga.

3:Mandonga ni yako sifa,
Kongole kwako mshefa,
Na kwa Tanzania sifa,
Hongera sana Mandonga.

4:Wanyonyi mpenda sifa,
Na Kenya yake kakufa,
Ni kama ana kifafa,
Hongera sana Mandonga.

Lwaga Mwambande (KiMPAB)
lwagha@gmail.com 0767223602

Post a Comment

0 Comments