Mheshimiwa Mchengerwa amaliza mgogoro Rufiji

NA JONH MAPEPELE

WANANCHI wa eneo la Nyanda na Utunge wilayani Rufiji wamemshukuru Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mbunge wa Rufiji na MNEC wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa kutatua mgogoro wa muda mrefu baina ya mwekezaji wa mradi wa uzalishaji wa sukari na wananchi wa maeneo hayo.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mkutano wa wananchi na Mhe. Mchengerwa kwenye eneo la Nyanda, Mwenyekiti Mstaafu wa Kijiji hicho, Amir Omary Magulu amempongeza Mhe. Mchengerwa kwa busara na jitihada zake za kuumaliza mgogoro huo ambao ulikuwa sugu kwa muda mrefu sasa.
Amesema mgogoro huo baina ya mwekezaji huyo ambaye ni Lake Agro unatokana na ukiukwaji wa makubaliano ya awali ya kupewa eneo la uwekezaji na kutopata taarifa sahihi za uwekezaji.
Akitoa suluhisho la mgogoro hilo, Mhe. Mchengerwa ameuomba uongozi wa Wilaya na Halmashauri ya Rufiji kuja kwa wananchi pamoja na mwekezaji ili kujadili kwa uwazi uwekezaji huo ili kurekebisha tofauti hizo na kuendelea kutekeleza mradi huo mkubwa wa pili nchini wa uzalishaji wa sukari.

Post a Comment

0 Comments