Okwa kutoka Simba SC apewa kandarasi ya mkopo Ihefu FC

NA DIRAMAKINI

KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Simba SC, Mnigeria Nelson Okwa amejiunga na klabu ya Ihefu FC kwa mkataba wa mkopo mpaka mwisho mwa msimu huu.
Okwa (26) raia wa Nigeria amekuwa na wakati mgumu kupata namba ya kudumu tangu atue Simba SC mnamo Agosti 4, 2022 kutokea klabu ya Rivers United ya Nigeria.

Simba SC ilifikia makubaliano ya kumsajili kiungo huyo mshambuliaji kutoka Rivers United ya Nigeria kwa mkataba wa miaka miwili.

Okwa ambaye anatumia mguu wa kushoto anaweza kucheza nafasi zote kwenye ushambuliaji na kwa ufanisi mkubwa.

Msimu uliopita Okwa ambaye alikuwa Rivers alifunga mabao manne na kusaidia kupatikana kwa mengine manne.

Okwa pia amewahi kuichezea Goround FC akiwa nahodha ambapo msimu wake wa mwisho mwaka 2019 alifunga mabao nane na kusaidia kupatikana kwa mengine matano.

Awali alipojiunga na klabu Simba, Okwa alitakiwa kujiunga na wenzake katika kambi ya maandalizi nchini Misri, lakini suala la vibali lilishababisha kushindikana kwa hatua hiyo.

Aidha,Okwa aliungana na Moses Phiri, Augustine Okrah, Victor Akpan, Habib Kyombo, Nassor Kapama na Mohamed Ouattara ambao walisajiliwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news