OR-TAMISEMI yatekeleza agizo la LAAC

NA ANGELA MSIMBIRA

OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) imetekeleza agizo la Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) la kujengea uelewa kuhusu matumizi ya Mifumo kwa Taasisi zinazofanya kazi na wizara hiyo.

Hayo yamebainishwa Januari 9,2023 na Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia masuala ya TAMISEMI, Ramadhani Kailima wakati akifunngua mafunzo ya siku tano kuhusu utekelezaji wa Mfumo wa ukusanyaji wa Mapato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wa LGRCS na TAUSI yaliyofanyika jijini Dodoma.

Amezitaja taasisi hizo kuwa ni Ofisi ya Mashitaka, Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mamlaka ya Serikali Mtandao (Ega), Polisi , Wizara ya Fedha, Ofisi ya Waziri Mkuu na Tume ya Utumishi wa Umma

Amesema kuwa, lengo la mafunzo hayo ni kujenga uelewa wa pamoja kuhusu Mfumo wa Ukusanyaji wa Mapato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGRCS) ambao unaenda kufungwa na mfumo wa TAUSI ambao unaenda kuanza kazi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ambapo mpaka sasa halmashauri 54 zimeanza kuutumia mfumo huo.

Kailima amefafanua kuwa, uelewa wa pamoja wa utumiaji wa mifumo ya TEHAMA katika ukusanyaji wa mapato utasaidia ufuatiliaji, ukaguzi, uchunguzi, kufungua mashitaka na kuiwezesha Serikali kuwa na ushahidi wa kutosha utakaowezesha kupeleka mashitaka na kuwezesha kuchukua hatua stahiki kwa watakaotuhumiwa kukiuka taratibu na miongozo ya ukusanyaji wa mapato kupitia mifumo ya ukusanyaji wa mapato iliyoanzishwa.

Ameeleza kuwa mafunzo hayo yatawawezesha kusikiliza hoja na kuweza kutoa maoni jinsi ya kuboresha mifumo hiyo lengo ni likiwa ni kuhakikisha mapato yanakusanywa kwa kufuata sheria na taratibu za fedha

Naye Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Erick Kitali ameeleza kuwa tangu mwaka 2014/2015, Ofisi ya Rais TAMISEMI ilianza kutumia mifumo ya Kielekroniki katika kukusanya Mapato ambao ulikuwa ukijulikana kama Local Government Revenue Collection System (LGRCS) na umetumika kwa muda wa miaka saba lakini kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia , Sera mbalimbali na mahitaji ya watumiaji imeonekana kuna umuhimu wa kuboresha mfumo huo.

Aidha, amesema katika bajeti ya Mamlaka za Serikali za Mitaa ya mwaka 2022/23 imeongezeka kutoka bilioni 860 hadi trilioni 1.01 kutokana na ongezeko hilo Serikali iliona umuhimu wa kuboresha mifumo na kuanzisha mfumo wa TAUSI.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news