Prof.Muhongo ana jambo na wakuu wa shule jimboni

NA FREESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara, Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo, ameomba kufanya kikao maalum na wakuu wa shule za sekondari zote 27 jimboni humo.

Hayo yamebainishwa leo Januari 30, 2023 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa jimbo hilo la Musoma Vijijini. Ambapo taarifa hiyo imeeleza kuwa kikao hicho kitafanyika Ijumaa ya Februari 3. 2023 kuanzia majira ya saa 3:00 asubuhi katika Shule ya Sekondari Busambara katika Kijiji cha Kwikuba.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa, ajenda ya kikao hicho ni "mapendekezo ya uboreshaji wa kujifunza na kufundisha kwenye sekondari" jimboni humo.

"Sekondari 27 ambapo 25 za Kata/Serikali 2 za "private" (KATOLIKI & SDA tarehe ya kikao ni Ijumaa, 3.2.2023 muda saa 3 :00 asubuhi Busambara Sekondari Kijijini Kwikuba ajenda ya kikao ni mapendekezo ya 'uboreshaji wa kujifunza na kufundisha kwenye sekondari zetu. Wakuu wa shule waje na Matokeo ya Mitihani ya Form II (2022, 2021, & 2020) na Form IV: (2022, 2021 & 2020)"na Matokeo ya form IV (2022) ya Sekondari 5,"imeeleza taarifa hiyo.

Aidha taarifa hiyo imesema kuwa, Mheshimiwa Mbunge Prof. Muhongo atafanya kikao kama hicho na wakuu wa shule zote za msingi 118 za jimboni humo ambapo tarehe ya kikao hicho itapangwa.

"Mbunge huyo atagharamia usafiri, chakula. Elimu ni nguzo muhimu ya taifa, elimu ni uchumi, elimu ni maendeleo,"imeeleza taarifa hiyo.

"Matokeo ya Sekondari tano za jimboni mwetu yameambatanishwa hapa Sekondari tatu za kata ya Etaro, Kiriba & Makojo Sekondari 2 za "Private" (Bwasi -- SDA & Nyegina - KATOLIKI),"imefafanua taarifa hiyo.





Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news