Rais Dkt.Samia afanya Mabadiliko ya Nafasi za Uongozi Serikalini leo Januari 3, 2023

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya nafasi za uongozi katika Serikali kama ifuatavyo:

Mosi, Rais Samia amemteua Balozi Hussein Othman Katanga kuwa Balozi wa Tanzania mjini New York, nchini Marekani na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa. Balozi Katanga anachukua nafasi ya Balozi Profesa Kennedy Gaston ambae uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huu balozi Katanga alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Pili, Rais Dkt. Samia amemteua Bw. Moses Mpogole Kusiluka kuwa Katibu Mkuu Kiongozi. Kabla ya Uteuzi huo Bw. Kusiluka alikuwa Katibu Mkuu Ikulu.

Tatu, Rais Dkt. Samia amemteua Kamishna Diwani Athumani Msuya kuwa Katibu Mkuu Ikulu. Kabla ya uteuzi huo Kamishna Diwani alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Wakati huo huo,Rais Dkt.Samia amemteua Bw.Said Hussein Masoro kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa. Kabla ya uteuzi huo Bw. Masoro alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Shughuli za Ndani wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 3, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi,Zuhura Yunus imeeleza kuwa, uteuzi huu unaanza mara moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news