Rais Dkt.Samia ametupa nguvu,ujasiri na ari ya kusonga mbele kila mmoja awajibike-Mwinjilisti Temba

NA MWANDISHI WETU

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia ni Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Bonifance Temba amesema, ujumbe wa kuaga mwaka 2022 na kuukaribisha mwaka 2023 uliotolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan umewapa nguvu, ujasiri na ari ya kusonga mbele ili kustawisha uchumi wa Taifa letu.

Temba ambaye pia ni mchambuzi wa siasa na uchumi ndani na nje ya nchi amesema, ni jambo la kutia moyo kuona kuwa miradi mingi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia inatekelezwa kwa ufanisi na kasi kubwa.

...ametutia moyo, kwamba mwaka huu utakuwa mzuri tuendelee kuvumiliana na tuendelee kuwa kitu kimoja, kwa sababu mwaka huu utakwenda kuwa mzuri.

Ninataka niwaambie kitu kimoja, hii miradi mikubwa, miradi ambayo unaona ya Bwawa la Mwalimu Nyerere, miradi ya reli ya kisasa, madaraja, barabara na vitu vingine vinavyofanyika vikubwa, vimeshafikia zaidi ya asilimia 75, kwa hiyo matumizi ya fedha kwenda nje yamepungua sana.

"Kinachobaki sasa ni mzunguko wa fedha ndani ya nchi, hivyo mzunguko wa fedha ndani ya nchi unaenda kuwa mkubwa.

"Na sasa hivi tunayo taarifa ya majira ya mvua kuwa, mwaka huu yatakuwa mazuri nchi nzima, nipende kuwatia moyo na kuwakumbusha wakuu wa wilaya na mikoa kwamba waendelee kuhamasisha wananchi huko mikoani ili waweze kulima sana mwaka huu.

"Ili chakula kiweze kuwa kingi sana, ili ikifika mwezi wa sita, wa saba na wa nane, na mzunguko wa fedha unakuwa mkubwa nchini. Lazima bei itashuka chini, kwa sababu vyakula vitakuwa vingi.

"Nataka niwaambie Watanzania, hakuna shida yoyote, shida iliyokuwepo ni shida ya Dunia nzima, Marekani wanalia, Sweden wanalia, hata gharama ya kununua gesi kwa ajili ya baridi ilkuwa ni shida, walikuwa wanaiomba Serikali iwasaidie.

"Kule Australia wanalalamika, nimeongea na watu wa kule,shida imekuwa kubwa, wananchi wameiomba Serikali iwasaidie kwa ajili ya baridi. Kwa hiyo ili si suala la Tanzania tu, ni suala la Dunia.

"Lakini kwa sababu chakula kinakwenda kuwa kingi na mzunguko wa fedha kuwa mkubwa, Watanzania tutaweza kuona vitu vinatulia, na miradi inaisha,safari zitakuwa rahisi. Na gharama itashuka na umeme hautakatika tena, kwa hiyo nina imani kabisa kwamba mwaka huu kama Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassana alivyotabiri unakwenda kuwa mzuri tuvumilie, na mimi kama kada mwadilifu Alphonce Temba kutoka Kilimanjaro ninawashauri Watanzania, tuvumilie, Mama anaupiga mwingi na anafanya kazi vizuri,"amefafanua Temba.

Kwa nyakati tofauti wana CCM mkoani Kilimanjaro wamesema kuwa, Temba ni miongoni mwa makada wachache ambao wamekuwa na misimamo thabiti kwa ustawi wa chama hicho licha ya kufanya mambo mengi ndani ya chama kimya kimya kwa miaka mingi.

"Mwinjilisti Alphonce Boniface Temba ni mtu mwenye uongozi wa kweli ndani yake, mkweli na asiyependa kuona mtu anakawisha juhudi za maendeleo zinazofanya na Serikali iliyopo madarakani ambayo imeundwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

"CCM, karne hii kinahitaji watu wenye vipaji vya uongozi na si waoga kusema mambo makubwa na wenye mvuto mkubwa kujenga hoja kama Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba, ambaye mara ya mwisho alionekana akigombea nafasi ya UNEC Taifa katika mkutano mkuu mwishoni mwa mwaka viti 20 bara, lakini kura hazikufika hata hivyo Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kulirudisha jina lake,"amefafanua Gervas Julius mkazi wa Vunjo.

Kupitia mkutano mkuu uliofanyika mwanzoni mwa mwezi Desemba, 2022 ndugu Alphonce Temba alikuwa kati ya makada walioomba zaidi ya elfu moja na mia sita na alikuwa kati ya waliofanikiwa kufuzu hatua zote, ingawa mwishoni kura hazikutosha

Mbali na hayo, Mwinjilisti Alphonce Temba ameshawahi kuomba kuteuliwa kuwania ubunge Jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro kupitia Chama Cha Mapinduzi mwaka 2015 ingawa kura hazikutosha.

Pia aliwahi kugombea nafasi ya Uenyekiti wa CCM Mkoa Kilimanjaro mwaka 2017 baada ya Halmashauri Kuu ya Taifa kulirudisha jina lake na kugombea tena mwaka 2022. Aidha, aliomba kugombea nafasi ya uenyekiti Wazazi Taifa ambapo jina halikurudi mwaka 2022.

Akizungumzia sababu za kujitokeza mara nyingi kuomba kuchaguliwa katika nafasi mbalimbali za uongozi katika chama, Mwinjilisti Temba amaesema ni kutokana na yeye wito wa uongozi alio nao ambao anatamani kutumia karama hiyo kuweza kustawisha chama kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.

"Wako watu wengi ndani ya CCM wenye vipaji, lakini hawabahatiki kuchaguliwa...,lakini wanaopata nafasi za uongozi wengi hawazifanyii kazi, wanageuka kuwa sehemu ya kulalamikia mambo, wito umetolewa kwa wenye nafasi ndani ya chama kukisemea chama na Serikali hasa kipindi hiki cha uhuru wa habari na milango ya mikutano ya hadhara imefunguliwa.

"Sisi tunaojua siasa za Kaskazini ambapo ndipo ngome kubwa ya upinzani nchini, chama kinahitaji viongozi wenye uwezo wa ushawishi kwa jamii na ujasiri katika kutenda mambo pamoja na umoja hili kuleta ushindi mkubwa kwa CCM mwaka 2024 Serikali za Mitaa na mwaka 2025 Uchaguzi Mkuu,"amefafanua Mwinjilisti Temba.

Aidha, wana CCM wameshauri kuliko kuchukua makada wa upinzani wakati umefika kuwamulika makada makini wenye vipaji nchi nzima ili kukisaidia chama kuelezea utekelezaji wa Ilani ya CCM na utekelezaji wa miradi mingi ya maendeleo inayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Wamesema,kwa miradi yote takwimu zipo ni suala la kuwaelimisha wananchi kwa urahisi, kwani jukumu hilo wameachiwa viongozi wa kitaifa tu, kwa kufanya hivyo imeelezwa kuwa, kazi ya CCM kushinda itakuwa rais sana katika chaguzi zote za mbeleni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news