MHESHIMIWA SAGINI AWATAKA WAKUU WA SHULE BUTIAMA KUTUNZA MAZINGIRA, KUPANDA MITI

NA DIRAMAKINI

MBUNGE wa Jimbo la Butiama Mkoani Mara ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Jumanne Sagini amewataka wakuu wa shule zote Jimboni humo kuhakikisha wanasimamia utunzaji wa mazingira ya shule wanazozisimamia ziwe katika hali ya usafi sambamba na kushiriki kikamilifu kupanda miti katika maeneo ya shule na kuitunza iweze kukua.
Mheshimiwa Sagini, ametoa kauli hiyo Januari 6, 2022 baada ya kutembelea Shule ya Sekondari Kigoma Malima iliyopo Kata ya Sirori Simba wilayani Butiama na kukuta mazingira ya shule hiyo si rafiki kwa wanafunzi kusoma kwa ufanisi zikiwa zimesalia siku chache shule kufunguliwa na wanafunzi warejee kuendelea na masomo yao.
Mheshimiwa Sagini, anaendelea kufanya ziara jimboni humo akiwa ameambatana na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi pamoja na wataalamu mbalimbali wa idara Halmashauri ya Wilaya ya Butiama.

Ambapo amesisitiza kuwa mazingira mazuri na rafiki yanasaidia wanafunzi kujisomea kwa ufanisi na kuwafanya wavutiwe zaidi kupenda kuwepo shuleni muda wote wa masomo pamoja na kuwajengea hali ya kuwa watunzaji wa mazingira katika jamii kwani wakiwa na msingi huo watauendeleza.
Pia Mheshimiwa Sagini, aliweza kubaini changamoto ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ambavyo vilijengwa chini ya kiwango katika shule hiyo na kuhitajika kufanyiwa ukarabati licha ya kuwa, havijatumika kwa muda mrefu tangu vilipoanza kutumika.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama, Karani Ruhumbika, amemuagiza mkuu wa shule hiyo kuhakikisha anasimamia na kutekeleza majukumu yake ya kazi kikamikifu na kufuata sheria na taratibu za nchi na kusema atazidi kufatilia kwa karibu kuhakikisha yote aliyoelekezwa iwapo ameyatekeleza kwa wakati.
Naye Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Butiama, Christopher Marwa Siagi alisema kuwa, ujenzi wa vyumba vya madarasa ni mkakati wa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi hivyo ni vyema wakasimamia utendaji kazi kwa kiwango cha hali ya juu ili kuepusha gharama zinazotumika kwa ukarabati zisaidie kuanzisha au kukamilisha mahitaji mengine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news