Rais Dkt.Samia asisitiza uwezeshwaji wa vijana kupitia umiliki wa ardhi

DAKAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema Serikali imetenga hadi eka 10 kwa kila kijana mwenye sifa ambapo baadae watazimiliki.

Rais Dkt.Samia amesema Tanzania iko katika mchakato wa kupokea maombi kwa kundi la kwanza la vijana watakaopata fursa ya kupata mafunzo ya miezi mitatu kuanzia katikati ya mwezi Februari halafu wagaiwe ardhi.
Hayo yamesemwa na Rais Dkt.Samia akijibu swali kuhusu namna ya kuvutia vijana kwenye kilimo, upatikanaji wa ardhi, teknolojia na fedha wakati wa ufunguzi wa mkutano unaohusu Kilimo unaofanyika Dakar nchini Senegal.

Pamoja na serikali kujidhatiti, Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB imetangaza kutoa mkopo wa dola za Kimarekani milioni 120 kwa ajili ya sekta ya kilimo ikiwemo umwagiliaji na kujenga kituo cha usafirishaji na usambazaji mbolea

Mpango huo unaolenga vijana na wanawake ujulikanao kwa jina la BBT, ‘Ujenzi wa Kesho Bora’ umeanzisha mfuko wa dhamana kwa vijana na huduma za mikopo nafuu chini ya Mfuko wa Pembejeo.

Rais Dkt.Samia amesema Tanzania imeamua kuanzisha mpango huo kutokana na idadi kubwa ya vijana kukosa sifa zinazohitajika na taasisi za fedha wanapoomba mikopo.

Tangu kuanzishwa kwa mpango huo wa BBT miezi sita iliyopita, tayari imeweza kutenga jumla ya eka 600,000 kwa nchi nzima na shughuli ya kusafisha mashamba hayo imeanza

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news