Rais Dkt.Samia ateua viongozi nane

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Januari 16, 2023 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi,Zuhura Yunus.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Prof. Ahmed Mohamed Ame kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA).

Prof. Ame anachukua nafasi ya Mhandisi John S. Nduguru. Prof. Ame ni Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Pili, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Bw. Eliud Betri Sanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Airtel Tanzania. Bw. Sanga anachukua nafasi ya Gabriel Malata aliyeteuliwa kuwa Jaji.

Bw. Sanga ni Mkurugenzi wa zamani wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSF).

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Samia amemteua Jaji (Mstaafu) Mathew Pauwa Mhina Mwaimu kuwa Mwenyekiti na Bw. Mohamed Khamis Hamadi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kipindi cha pili.

Aidha, Rais Samia amewateua Makamishna wa Tume kama ifuatavyo:-

>Bw. Thomas Paulo Masanja, kuwa Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora.

>Bi. Amina Talib Ali, kuwa Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora.

>Bw. Khatibu Mwinyi Khatibu, kuwa Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora.

>Bw. Nyanda Josiah Shughuli, kuwa Kamishna wa Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, utuezi huu ni kuanzia tarehe 15 Januari, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news