RC Mtaka: Kesho Njombe tuna jambo kubwa

NA DIRAMAKINI

MKUU wa Mkoa wa Njombe, Mheshimiwa Anthony Mtaka amesema, kesho Januari 5,2023 wanatarajia kuwa na mkutano mkubwa wa wafanyabiashara huku mgeni rasmi anatarajiwa kuwa ni Mheshimiwa Dkt. Ashatu K. Kijaji (Mb), Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara.
"Januari 5, 2023 siku ya Alhamisi kuanzia saa nne kamili asubuhi kutafanyika kikao kikubwa cha Sekta Binafsi ya Mkoa wa Njombe (Wafanyabiashara wa Makundi yote) na uongozi wa Serikali ya mkoa.

"Mgeni rasmi asmi katika mkutano huu mkubwa atakuwa Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt.Ashatu Kijaji,"amesema.

Mkutano huo utafanyika Ukumbi wa Halmashauri ya Njombe Mji.

"Wafanyabiashara wote wanakaribishwa, lengo ni kutatua kero za sekta binafsi ndani ya mkoa na kuona biashara ndani ya mkoa zikikua na kustawi. Sekta Binafsi ni muhimili wa ajira na uchumi ya mkoa na nchi yetu,lazima ilindwe na kuheshimiwa na wadau wote wanaosimamia maamuzi ndani ya mkoa.Mkutano huu utarushwa LIVE(Mubashara) na TBC -Tv,Radio na Mitandao ya Kijamii,"amesisitiza RC Mtaka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news