Saba wapewa jukumu muhimu BAKWATA

NA DIRAMAKINI

MUFTI wa Tanzania Shekh Dkt.Abubakari Zubeir Ali ameunda tume ya maboresho ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), yenye wajumbe saba.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na BAKWATA na kusaini na Sheikh Dkt. Ally imeeleza kuwa, tume hiyo ameiunda kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Katiba ya Baraza Kuu la BAKWATA, kipengele 84:17.

Wajumbe walioteuliwa kuwa ni Sheikh Issa Issa ambaye ni mwenyekiti na katibu wa tume ni Alhaji Omar Ege. Wajumbe wengine ni Alhaji Nuhu Mruma, Daudi Nasibu, Iddi Kamazima, Mohamed Nyengi na Qussim Jeizan.

Wajumbe wa tume watafanya kazi kwa kufuata hadidu saba ambazo zinatajwa kwenye taarifa hiyo kuwa ni kuhakiki madeni ya BAKWATA na kushauri namna ya kuyalipa, kufanya uchunguzi wa mali za BAKWATA ambazo zinamilikiwa na watu wengine kinyume cha taratibu na kuchukua hatua za kutatua na kufanya tathimini ya changamoto za mifumo ya utawala inayoikabili BAKWATA na kushauri namna bora ya kufanya maboresho.

Pia watawajibika katika kufanya uchunguzi wa mikoa au wilaya zenye migogoro mikubwa ya uongozi au mali na kuchukua hatua kuitatua, kuibua na kubuni vyanzo vipya vya mapato kwa BAKWATA na masuala mengine muhimu ambayo tume itaona yanafaa kufanyiwa kazi kwa ustawi bora wa baraza hilo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news