Prof.Muhongo aongeza kasi maboresho Sekta ya Elimu Musoma Vijijini

NA FRESHA KINASA

MKAKATI wa kuendelea kuimarisha Sekta ya Elimu katika Jimbo la Musoma Vijijini mkoani Mara unaendelea kufanywa na Mbunge wa jimbo hilo, Mheshimiwa Prof. Sospeter Muhongo ambapo anatarajia kuendesha harambee kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Muhoji katika Jata ya Bugwema siku ya Januari 24, 2022.

Hatua hiyo ni mwendelezo wa mikakati yake, Prof.Muhongo pamoja na Serikali katika kuimarisha sekta ya elimu na kuhakikisha sekta hiyo inakuwa thabiti kuwezesha kuchochea kasi ya maendeleo na uchumi kwa Watanzania.

Hayo yamebainishwa leo Januari 22, 2023 kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge ambapo imeeleza kuwa, "Harambee ya ujenzi wa Muhoji Sekondari itafanyika siku ya Jumanne tarehe 24 Januari 2023 muda saa 8:00 mchana, mahali ni Kijiji cha Muhoji katika Kata ya Bugwema,"imeeleza taarifa hiyo na kuongeza kuwa.

"Karibuni tuungane na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, kuchangia ujenzi wa Sekondari mpya kwenye Kijiji cha pembezoni mwa Kata ya Bugwema. Bugwema Sekondari hii ni Sekondari ya Kata ya Bugwema yenye vijiji vinne vilivyoko mbalimbali, imeelemewa. Wanafunzi wa kodato cha kwanza 2023 ni 362." imeeleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,Form I (2023) ina Mikondo saba (7) Jumla ya Wanafunzi ( FI-FIV) ni 740 huku walimu wakiwa ni 10.

Aidha, taarifa hiyo imefafanua kuw,a mchango wako unaweza kuupeleka kwa Mtendaji wa Kijiji (VEO) Kijiji cha Muhoji simu 0686 557 264. "Lengo letu Muhoji Sekondari ifunguliwe Januari 2024, elimu ni uchumi, elimu ni maendeleo," imeeleza taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news